Wednesday, January 20, 2016

SOMO: USIFURAHIE KUSHINDWA KWA MWENZAKO.


Shalom people of God...............!
Sidhani kama mko njiani na rafiki yako mnatembea alafu gafla rafiki yako akateleza kwenye matope na kuanguka chini alafu ukaanza kumcheka badalaa ya kumpa pole na kumsaidia kunyanyuka! sidhani. na wala sijawai kuona katika maisha yangu.
wapo watu leo wanafurahia kuanguka au kushindwa kwa wenzao. yawezekana ni chuoni,matokeo yametoka ukasikia mwenzako ana supplementary au kadisco, kwako inakuwa sherehe. au kanisani au mahali mnapoishi. upo masemo usemao leo kwangu kesho kwako!! waswahili wamesema ila kiukweli kauli hii au msemo huu una ukweli ndani yake kabisa.
Mika 7:8 inasema" usifurai juu yangu, ee adui yangu. niangukapo nitasimama tena nikaapo gizani bwana atakua nuru kwangu" namshukuru dada yangu Upendo nkone aliimba nyimbo hii na pengine unaipenda sana lakini hufuati yale yalioimbwa kwa maana bado unafurai juu ya kushindwa kwa mwenzako. hapa mika anasema usifurai juu yangu, maana nitasimama tena. leo hii jambo hili limekuwa hodari sana,waswahili wamesema tena si kila akuchekeaye ni rafiki yako! inawezekana unacheka na mwenzako, mnapiga stori na inawezekana mwenzako anajua unampenda kupita maelezo maana unamwonesha hivyo, lakini moyoni bado unataka na unatamani ashindwe, bado unamnenea mabaya.
kuna watu hawapendi mafanikio yako na wanakesha wakiomba ushindwe. unaweza ukawa shaidi wa hili ninalosema maana tunaona hata kwenye maigizo, kuna watu wanaenda kwa waganga kulogana au hata kuuana kisa kwanini amemzidi mafanikio. ndugu huyu Mungu tunayemwabudu hana Roho mbaya kiasi hicho! iweje sisi?
Wagalatia 6:1 inasema"ndugu zangu mtu akighafilika katika kosa lolote ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole ukiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. kugafilika ni kuwa katika hali ya kusahau au kupitiwa. paulo anaawambia wagalatia kuwa mtu akijisahau au kupitiwa kwa kosa lolote nyie mrejezeni. hapo juu nimesema inawezekana kanisani kuna wanaofurai kuona fulani amesimamishwa huduma kisa amefanya dhambi ya uzinzi. na pengine ulikuwa unamwona kwamba hali yake ya kiroho inashuka, je ulichukua hatua gani kumrejeza? watu siku hizi tuko tayari kumuacha mwenzetu apotee, na hiyo ni sababu ya kutokuwa na upendo ndani yetu. nilianza kwa mfano pale juu kwamba unaweza ukamwacha nakumcheka rafiki yako aliye anguka kwenye matope njiani?
Yakobo 5:19-20 inasema " ndugu zanngu ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli na mtu mwingine akamrejeza 20 jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke ktk njia ya upotevu ataokoa roho na mauti na kufunika wingi wa dhambi.
Naupenda sana mstari wa 20 yaani anasema utakuwa umeokoa roho na mauti na kufunika wingi wa dhambi. kwaiyo unapowarudisha wenzako kundini anasema umeokoa roho na kufunika wingi wa dhambi. sasa tatizo linakuja sisi wala hatujali inawezekana una rafiki yako unaona kabisa anapotea hayuko katika njia, wewe ndio kwanza hata ujali tena unasubiri kuona mwisho wake! wapo watu wenzao wakishashindwa utasikia "mi nilijua tu lazima yangetokea haya" Ndugu kama ulijua ulikuwa wappi kumuonya?? umesubiri mambo yaaribike ndio useme?
Usifurahie kushindwa kwa mwenzako, unaapo ona mambo hayaendi sawa kaa naye, jaribuni kuyaweka vizuri kama maandiko yanavyosema ktk yakobo na wagalatia.jua kwamba linalompata mwenzako leo nani ajuaye laweza kukupata kesho!
STAY INSPIRED!!!!!!!

1 comment:

  1. Sands Casino Resort | Slots, Poker, Table Games & More
    At Sands Casino Resort in Las Vegas, we're the 제왕카지노 locals' only casino resort offering a variety of slot, septcasino video poker, keno and video poker 메리트카지노총판 to its guests.

    ReplyDelete