Bwana yesu apewe sifa, Hamjambo na karibuni katika mwendelezo wa masomo yangu.Leo ninalo somo kama linavyosema hapo juu, kwamba ni lazima kuwa na neno la Mungu ili tuweze kushinda.
Kwanza kabisa neno ni Mungu mwenyewe, soma Yohana 1:1''Hapo mwanzo kulikuwako neno, naye neno alikuwa Mungu. Kwaiyo, tunadhiirishiwa kwamba neno ni Mungu. kwa mantiki hiyo sasa tunaona kuwa kumbe kuwa na neno ni kuwa na mungu mwenyewe.
Wengi hatujajua kuwa neno ni mungu na kama tunajua sidhani kama wakristo wa sasa tusingependa kusoma neno. Mimi nashangaa sana, yaani sijui mkristo anaishije eti siku inapita hajasoma neno, kwa upande wangu hua najisikia vibaya sanaaaa. Sikatai zipo sababu zinakubana inapita siku hujasoma neno....sawa! ila hakikisha hiyo sababu kweli inakubalika na Mungu na kwa mkristo aliyesimama kweli kweli lazima aumie ndani au aone utofauti. kama wewe unaona kawaida basi tambua iko shida ndani yako.
Tuanze kwa kusoma Mathayo 22:29 inasema''Yesu akajibu akawaambia, mwapotea kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa mungu''. Kwaiyo kumbe hawa masadukayo walikua wanapote akwa sababu yakutokujua maandiko. vipi wewe na mimi ambao leo imekua shida kusoma neno la Mungu, alafu bado unataka eti Mungu akuokoe na majaribu yanayokusonga? sikia Yesu alipokuwa akijaribiwa na ibilisi nyikani, alimshinda kwa neno tu...soma Mathayo 4 kuanzia mstari wa kwanza, utaona kila alipokua anajibu alikua ana refer kwenye maandiko. Sasa unaweza ukaona kumbe hata Yesu ambae angeweza na alikua na uwezo wa kumkemea tu shetani na aondoke ila bado nayeye alihitaji neno ili aweze kushinda sembuse mimi na wewe??????
Ukisoma tena Zaburi 119:11 inasema''moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije nkakutenda dhambi'' Daudi alijua kuwa neno la Mungu likikaa ndani yake si rahisi kwake kuanguka dhambini. ukisona mstari wa 9 inatuambia kuwa ni kwa jinsi gani kijana atasafisha njia yake.......ni kwa kufuata na kutii neno lake. Kwaiyo utalitiije neno la Mungu kama usomi? Kwaiyo bado tunaona umuhimu wa neno yaan Mungu katika maisha ya ushindi.
Katika waefeso 6:16-17 inasema'' ipokeeni chepeo ya wokovu na upanga ambao ni neno la Mungu''. Sasa unahitaji nini tena maana vita vyetu si juu ya damu na nyama, kwaiyo kumbe kama skari vitani ukiwa na neno your fully equiped yaan kama ni bunduki unayo, magwanda umevaa, begi la kubebea vitu unalo, mabuti unayo, upanga unao n.k...... Ukisoma Joshua 1:8 uataona kwa anasisitiza kuwa na neno na kulitafakari ila nimefurahishwa anaposema '' Ndipo utakapostawi na kufanikisha njia yako.
Wapendwa wengi wetu hatuna biblia ambayo ndo silaha ya mkristo na bado wengine tunazo biblia lakini ni jumapili kwa jumapili yaani namaanisha unaisoma jumapili kanisani tena ni kufatisha tu yale asemayo Mchungaji ila baada ya pale ni hadi jumapili ijayo aukama kuna ibada siku za katikati. sasa tunategemea vipi kushinda???? sawa maombi ni silaha ila bila neno ni bure ni sawasawa na mtu ana bunduki ila haina risasi alafu yuko mstari wa mbele vitani!!!!! pata picha nini kitatokea.
Uko mfano wa watu fulani ambao walikua wanafunga ndoa yao. sasa wakati watu wanatoa zawadi, wengine wakatoa gari, friji, dressing table n.k. ila kuna jamaa mmoja yeye aliwazawadia Biblia, tena aliomba kwa mc na akaongea kuwa hana chochote ila kwa kuwatia moyo maharusi wale wakasome( akataja sura na kitabu wakasome). Maharusi walipofika nyumbani wakaiweka Biblia juu ya kabati na kuisahau. siku moja mama alipokua anasafisha kabati akaikuta na kuikung'uta maana ilikua na vumbi mno. alipokua ana kung'uta akakumbuka ile sura aliyowaambia yule jamaa wakaisome, la haula! si akakuta cheque........yule mama alifurai na kurukaruka , akamwita mumewe pia, mumewe alivyokuja walifurai sana.....baada ya furaha kupungua, jamaa si akaisoma vizuri! oooouuuuhh!!! kumbe tarehe ilikua ishapita. cheque ya milioni kumi! Huo ni mfano tu kwa jinsi gani hawa watu hawakuona umuhimu wa Biblia.
BE BLESSED YOU ALL......( stay inspired)
No comments:
Post a Comment