Bwana yesu apewe sifa wapenzi wasomaji.........napenda kumshukuru Mungu kwa nafasi alionipa tena, Katika mwendelezo wa masomo yangu, leo nitafundisha juu ya ni kwanini watu wa Mungu wengi hawabarikiwi.
Kwanza lazima tujue kuwa baraka ni haki yako kabisa kwa sababu ni ahadi ya Mungu mwenyewe, ukisoma kumb 28 utaona jinsi gani ahadi hizo zimetolewa. Sasa mtu unaweza ukajiuliza inakuaje nasema ni haki ya mwamini wakati wewe umekua ni Mtu wa kuwapigia makofi wenzio kanisani wakati wanashuudia baraka walizopata either Mungu kawasaidia kununua gari, kupata kazi, kujenga nyumba, n.k
Jibu ni rahisi sana....binafsi namshukuru Mungu kwa sababu amenifunulia siri hii na imekua msaada mkubwa sana katika maisha yangu.
Wapendwa sisi wenyewe ni chanzo cha kuzuia baraka hizi..........iko hivi, kama kuna kitu ambacho Mungu anapenda kutoka kwetu, basi ni utii wetu kwake(anapenda kuabudiwa, kuheshimiwa). Sasa tatito linaanzia hapa Mtu anataka Mungu ambariki wakati yeye hataki kumtii au kumheshimu. tusome Isaya 59:1-2''tazama mkono wa bwana haukupunguka hata usiweze kukuokoa wala sikio lake sio zito lisiweze kusikia, lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na Mungu na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Jamani haya maandiko nayapenda kwasababu yako wazi sana. yaani ukianzia mstari wa pili anasema, lakini maovu yenu na dhambi zenu zimeuficha uso wake na zimewafarakanisha. kwaiyo tunaona kabisa Mungu ashindwi kukubariki ila dhambi zako ni chukizo mbele zake na ndio kwazo la yeye kukubariki.
Tusome tene Isaya 1:19'' kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi'' bado anasisitiza kitu kimoja (UTII). kama nilivyosema hapo juu Mungu ndio kitu anapenda yaani ukimuheshimu ni lazima baraka zitakuja tu.
Saa nyingine sio lazima hata kuomba, naomba unielewe sisemi kwamba usiombe hapana maombi ni muhimu sana na ndio silaha yetu ila ukijishugulisha na Mungu , yeye anajishugulisha na wewe kwa mfano Mtoto akiwa watii kwa wazazi kiasi cha kumfurahisha, utakuta siku mzazi anampa Mtoto labda zawadi au hela ya matumizi bila hata ya Mtoto yule kuomba. mimi imewahi kunitokea naamini na baadhi yetu pia. 2Nyakati 7:14'' ikiwa Watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi zao na kuiponya nchi''. Haya hapa tuna vitu vitatu, moja ni kijinyenyekesha na kuomba, mbili ni kutafuta uso wa Mungu, tatu ni kuacha njia mbaya. yeye(Mungu) sasa atachofanya, atasikia, atasamehe dhambi na kuponya. Kwaiyo unaitaji nini zaidi maana hapa mstari uko wazi kabisa wajibu wako na wajibu wa Mungu kwako.
Zaburi 1:1-3 ukiangalia inasema ana heri mtu yule asiekwenda katika shauri la wasio haki, ukisoma biblia ya kiingereza inasema '' BLESSED IS THE MAN'' kwaiyo mtu asieenda katika dhambi amebarikiwa. mstari wa tatu unasema na kila alitendalo litafanikiwa............
Wapendwa mimi mwenyewe ni shuhuda wa mambo ninayo yasema wala sisemi tu kwa sababu Mungu amenipa somo hili, la hasha! baada ya kupewa somo hili nilijirekebisha pale nilipokosea na kwa kweli namuona Mungu sana katika Maisha yangu , kuna mambo najikuta yanatokea hadi nashangaa kwasababu hata mengine sikuomba ila nabaki kumshukuru.
Ndugu mpendwa nawasihi katika Bwana , ifike muda tuache sasa kumlaumu Mungu kwa sababu tatizo ni la kwetu wala si lake. mfano unamkuta mtu analalamika kwenye maombi yake, na ni wazuri sana kwenye kunukuu maandiko utasikia ulisema tutabarikiwa tuingiapo, tutokapo, litabarikiwa kapu langu!!! ungejua unaemlalamikia kwanza hata kukusikia akusikii ungeacha tu.....Kwaiyo ebu tubadikilike sasa tuache maovu na dhambi tunazofanya kwa hakika baraka zitatujilia, maana Mungu si Mwanadamu hata aseme uongo lazima atafanya.
BARIKIWA!!!!!
Oh Mungu akubariki mtumishi nikweli ahadi za Mungu ziko palepale lakini kanuni hazifuatwi
ReplyDeleteAsante kwa neno lako zur mtumishi.
ReplyDeleteNi kweli.Watumishi kwa Neno hili turudi sasa tujichunguze niwapi tumekwenda kinyume na mapenzi ya Mungu naturejee na kutengeneza.Mbarikiwe.Amina
ReplyDelete