Thursday, February 18, 2016

SOMO; JINSI YA KUWA MTU MZURI/ MWEMA MACHONI PA WATU.


Mwanzo 4:7 inasema" kama ukitenda vyema utapata kibali? usipotenda vyema dhambi iko mlangoni ina kuotea"
Kwaiyo ili ukubalike ni lazima kutenda mema.....hapa Mungu alikuwa akimwambia kaini.........ni dhahiri hata sehemu tunazoishi, unaweza jiuliza"mbona upati kibali kwa wenzako?? mbona unachukiwa?? hapa nimejaribu kukupa mbinu ambazo zitakusaidia kuwa mwema machoni pa watu..............fuatilia!
1 JIFUNZE KUACHILIA/ KUSAMEHE
hakuna kitu kinachomuumiza mtu kama yeye akikukosa alafu wewe ukasamehe na usilipize ubaya kwa ubaya. Petro aliambiwa na Yesu samehe saba mara sabini. siri kubwa ya kukufanya uonekane mwema sio tu kusamehe, na kuachilia pia. kuna msemo unasema "nimekusamehe ila sito kusahau" kumbuka kama na Mungu nae angekua anatumia huo msemo ni dhahiri wengi tungekua tunapokea kichapo kila siku. haijalishi ni adui yako, ndugu yako au mtu yeyote..wewe samehe na mwisho wa siku alie kukosea ataomba msamaha mwenyewe.
2 USIWE MTU WA HASIRA
hii inaweza kuendana na hapo juu, lakini tofauti ni kwamba utakiwi kuwa na hasira za hovyo hovyo hata ktk mambo ya kawaida. biblia inasema" hasira inakaa kifuani mwa mpumbavu" kuna watu wanaopenda kudhila dhila, kukasirika kasirika hata kama amekanyagwa bahati mbaya kwenye daladala basi atakasirika na kutupia maneno mengi na pengine matusi.
3 KUWA MWAMINIFU NA MKWELI
Watu watakupenda sana. mimi nina mifano mingi sana ya jinsi uaminifu ulivyo nisaidia watu kunipenda na kuniamini. hili nimeliona hata kwa wazazi wangu, wametokea kuniamini sana na upendo naona unazidi kiasi cha kwamba nikiomba chochote napewa na napewa ruhusa ya kufanya lolote maana wananiamini kwamba sitawaangusha.
4 WASAIDIE WENGINE
siri kubwa ya kukubalika, ni kusaidia jamii inayokuzunguka. najua mnamjua mohamed dweji, jiulize kwanini watoto wa singida wanampenda sana...ni kwa sababu amejikita kwenye kusaidia na kutoa. juzi mengi amesaidia walemavu na wenye shida usishangae kuona anependwa na kukubalika sana.unaweza usiweze kwenda kwa yatima na wajane lakini jamii tu inayokuzunguka, je unasaidia na kushirikiana nao?
5 WASIKILIZE WENGINE/USHAURI
Kuna watu wanapenda maamuz yao ndiyo yawe final...hawataki kusikiliza wengine. kuna msemo unasema "bora mbili kuliko moja" yanapokuwa mawazo mawili ni bora kuliko la kwako tu.na hii inatokea sana katika mahusiano, mume anapenda kuwa na maamuzi ya kipekeyake bila kumsikiliza mwezake.pia kwa kuwasikiliza wengine unajifunza mengi.
6 JITAMBUE 
Tunaishi katika dunia ambayo kuna watuhawajitambui kabisa. mwengine ana umri mkubwa ila mambo bado ni ya kitoto, kwa nini? ajajitambua! unaojitiambua ni rahisi sana mtu mzuri kwa jamii yako, hakuna apendaye utoto unaofanya hyo itaelekea watu kukudharau na kukuona mjinga. mfano wanaopenda sifa mbele za watu. na siku hizi watu huwa wanakuchekea ila moyoni hawakupendi hata chembe.
7 KUBALI KUSAHISHWA/MAONYO
wapo ambao hawapendi kabisa kuonywa. tambua hii inakusaidia kujua wapi umekosea na ujirekebishe, wengine wanaposaidiwa wanakasirika, namna hii ni ngumu kubadilika. 
8 JIHESHIMU/ HESHIMU WENGINE
dont expect to be respected if u dnt respect ur self. lazima kwanza ujiheshimu ndipo utaheshimiwa. heshimu wengine, siku hizi heshima kidogo kwa vijana ni F, ila hii inasaidia sana unapo heshimu watu wa jamii yako, unakubalika si na wakubwa tu hadi wadogo.
Mungu awabariki sana......tujaribu kufanya haya na nakuhakikishia lazima utakubalika tu maana huko ndiko kutenda Mema.
STAY INSPIRED!!!

No comments:

Post a Comment