Wapo watu waliorudi nyuma kwa sababu tofauti tofauti. wengine wamerudi nyuma kwa sababu wamekataa au wamekatishwa tamaa, wengine wamerudi nyuma sababu wanaona kuokoka kwao hakujawa na faida au msaada wowote katika maisha yao. Nataka utambue kitu kimoja mtu wa Mungu, inawezekana wewe ndio chanzo cha kurudi kwako nyuma!! wapendwa wengi leo tumezoa kusema "shetani amejiinua" katika kila jambo. Nataka ujue kuwa unaweza ukawa unamwendekeza shetani.
mfano, kumbuka kile kisa cha yusuph, laiti kama yusuph asingemkimbia mke wa potifa, basi angeanguka katika dhambi ya uzinzi.
Wagalatia 5:7 inasema " Mlikuwa mkipiga mbio vizuri, ni nani aliyewazuia msitii kweli" paulo alikuwa akiwashangaa wagalatia kwamba walikua wakisimama katika imani, sasa ni nini kilikuwa kimewatokea paka wakageuka au wakarudi nyuma. kama nilivyotangulia kusema hapo juu, kuna mwingine anaweza akaonaa kwamba kuokoka hakuna faida yoyote kwake.....kitu kingine wapendwa tunachokosea ni kufikiri kwamba ukisha okoka kila kitu kinanyooka HAPANA! unapookoka shetani hafurahii hata kidogo na unakuwa umetangaza vita na yeye kwaiyo sidhani kama ukiwa vitani huwa mambo yanakuwa mazuri!!! ni lazima kupambana ili uweze kushinda.
Hosea 14:1 inasema"ee israeli mrudie BWANA, Mungu wako maana umeanguka kwa sababu a uovu wako. nilitangulia pia kusema kuwa inawezekana ukawa chazo cha kurudi kkwako nyuma....hapa hosea anawaambia wana waisraeli wamrudie Mungu maana wameanguka kwasababu ya maovu wanayotenda. unajua Biblia inasema usiipende dunia wala mambo yalliyomo ndani yake katika 1 yohana 2:15, huwezi ukasimama wakati unaipenda dunia lazima dunia itakuvuta tu na mwisho wa siku utarudi nyuma.
Wagaltia 1:6 inasema" nastaajabu kwa kuwa mmemwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo na kugeukia injili ya namna nyingine" kuna wengine pia wamerudi nyuma na kugeukia injili ya namna nyingine. kwanza nataka kukwambia kuwa mahali ulipo upo mahali sahihi kabisa. wapo watu kila kukicha wao ni kuhama makanisa pengine wakitafuta miujiza n.k lazima utayumbishwa na upepo tuu. kuna manabii wa uongo hata Biblia inasema sasa kama we ni wa kuhamahama kwanini usinaswe?? na tatizo nililokuja kuligundua ni kwamba wakristo wa leo wanataka sana miujiza ya papo kwa papo. soma Yohana 5:1-9, kisa cha yule mtu ambaye alikuwa hawezi miaka thelathini na minane kwenye birika la Bethzatha. yeye akuwa na mtu wa kumuingiza kwenye birika ila kuna siku yesu alikuja akamkuta palepale na kumponya......ndivyo na wewe itakavyokuwa yesu atakukuta hapohapo na kukuponya huna haja ya kuhangaika, utapishana na muujiza wako bure.
Waebrania 10:31 anashangaa anasema kuwa ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai. ni sawasawa na mtu umeokota dhahabu alafu ukaja ukaitupa kwa sababu huitaki!! watu watakushangaa.......na wokovu ni wathamani sana, hivyo shikilia sana ulicho nacho.
katika ufunuo 2:5 inasema kumbuka ulipo anguka ukatubu, mpendwa kama ulianguka kwa sababu moja wapo ya hizo hapo juu ni vizuri na muda muafaka ukatubu. Mungu anasema nirudieni mimi, kwaiyo yuko radhi leo kukupoke ukirudi.Barikiwa
STAY INSPIRED!!!!!!
No comments:
Post a Comment