Tuesday, February 2, 2016

SOMO: USILALAMIKE, MKUMBUSHE MUNGU, YEYE NI MWAMINIFU ATAFANYA.


Shalom.........
Isaya 43:26 inasema" unikumbushe na tuojiane, eleza mambo yako upate kupewa haki yako" angalia kwa makini sana andiko hili lilivyo na nguvu........hapa Mungu anasema kwamba umkumbushe, muhojiane, ueleze mambo yako alafu upewe haki yako.
Maana ya HAKI ni, kitu au jambo ambalo mtu anastahili kupata. kwaiyo kwa maana nyinine ni kwamba Mungu amesema umkumbushe, muhojiane, ueleze mambo yako uweze kupewa stahili zako.
Je Mungu anasahau mbona anataka umkumbushe? tafsiri ya kingereza "NIV Bible" inasema " reviw the past for me, let us argue the matter together state the case for innocence" Mungu huwa ana kanuni, anataka tutende mema kwanza alafu ndipo na yeye atutendee sisi. ila wanadamu tumegeuza na kumtaka Mungu atutendee wema kwanza. kwa mfano ukisoma Yakobo 4:8 inasema " mkaribieni Mungu naye atawakaribia ninyi" sasa sisi tumegeuza na kutaka yeye ndo atukaribie. Kwaiyo anaposema umkumbushe, anataka umpe sababu za kwanini unataka kutendewa unayoomba.
Na hapo ndipo watu wengi tunapokosea sana, tunataka tupewe haki zetu toka kwa Mungu lakini at the same time sisi atumpi anayotaka, ukisoma Mika 6:8 utaelewa ninachosema. swali linakuja tena, Je unacho cha kumkumbusha Mungu???
Isaya 38:1-5, hii ni habari ya Hezekia. Mungu alimtuma isaya kwenda kumwambia kuwa lazima afe, ila napenda sana ule mstari wa 3, unasema " akasema, ee Bwana kumbuka haya, nakusihi kwamba nimekwenda katika kweli na kwa moyo mkamilifu na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. unaona alichofanya Hezekia ni kwenda kwa Mungu na "STRONG REASON OF WHY HE DOES NOT DESERVE TO DIE YET" Je unacho cha kumkumbusha Mungu kama Hezekia?
Mdo 9:36-43, Hapa tunaona habari za mtu aitwaye Tabitha tafsiri yake ni dorkasi, alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizotoa. alipokufa wale wajane na watu aliowasaidia walihuzunika sana, wakatuma ujumbe kwa Petro. sasa mstari wa 39 unasema" Petro akaondoka akafuatana nao. walipofika wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye wakalia na kuonyesha zile kanzu na nguo alizoshona dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. Mungu alimfufua dorkasi kwa sababu wale wajane walimwonyesha Petro juu ya matendo mema aliyofanya dorkasi naye petro alimkumbusha Mungu.
Inawezekana unalalamika sana majaribu yanapokusonga au unaona Mungu yupo mbali na wewe maana umeomba sana ila bado hujafanikiwa, pengine huna cha kumkumbusha Mungu. kama wewe ni mwaminifu kwa Mungu basi una kila sababu ya kumkumbusha juu ya jambo fulani naye atafanya. Hezekia aliweza kumkumbusha Mungu kwanini wewe ushindwe na umekuwa mwaminifu kwake??
ukisoma Waamuzi 6:13, Gideoni alilamika kwa Mungu akisema " ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo yote haya yametupata??? inawezekana umeshalalamika kama Gideoni lakini kumbe unachotakiwa ni kuacha kulalamika na kumkumbusha Mungu. hebu fikiria kama Hezekia angeanza kulalamika badala ya kumkumbusha Mungu, nini kingetokea??
ni muda mzuri wa kuendelea kuwa waaminifu kwa Mungu ili tuwe na kitu cha kumkumbusha hapo badae........"GOD IS A REASONABLE GOD"
Kama unafatilia masomo yangu unaweza ukanipata pia kwenye blog yangu "victorchubwablogspot.com.
au kwa mawasilino 0715918940........STAY INSPIRED!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment