Imefika sehemu tumetaka na kutamani baraka kutoka kwa Mungu na kujiuliza mbona mimi sibarikiwi! na pengine tunapokuwa katika shida vivyo hivyo lakini yamkini tukakata tamaa maana tuliona kama hakuna msaada. katika somo hili nataka tujifunze kitu kimoja kwamba ukitembe katika mapenzi yake, yeye ni mwaminifu hata kukufanyia mambo ya ajabu kama Yeremia 33:3 inavyosema.
Isaya 65:24 inasema" na itakuwa ya kwamba kabla hawajaomba nitajibu na wakiwa katika kunena nitasikia" unaona kumbe Mungu anajua haja ya mioyo yetu.......yaani kabla hata hujaomba yeye anajua unachotaka kumwambia. shida inaanzia hapa! wote tunajua kuwa dhambi ni chukizo mbele zake, sasa how do you expect him to have you blessed while unamchukiza???? kuna somo langu linaitwa "TUNAMZUIA MUNGU KUTUBARIKI KWA SABABU YA MAOVU YETU" kama utakuwa utataka kuelewa zaidi waweza kupitia blog yangu victorchubwablogspot.com.
Tusome tena Isaya 66:2b inasema" lakini mtu huyu ndiye ntakayemwangalia mtu monge, mwenye roho iliyopondeka(mnyenyekevu), atetemekaye asikiapo neno langu" tunazidi kuona kuwa kumbe Mungu anajishuguisha zaidi na wale wanaojishugulisha naye. siku hizi watu wamegeuza maandiko kwa mfano Yakobo 4:8 inasema "mkaribieni Mungu naye atawakaribia" sasa siku hizi imekuwa tofauti yaani watu wanataka Mungu ndo awakaribie kwanza.kwaiyo si rahisi kama unategemea kubarikiwa na kuponywa wakati hufanyi yaliyo mapenzi yake.
Zaburi 34:18-19 inasema" Bwana yu karibu na wao waliovunjika moyo na waliopondeka roho huwaokoa, mateso ya mwenye haki ni mengi lakini Bwana humponya nayo yote. napapenda sana hapa....embu jaribu kusoma kwa makini sana jinsi anavyosema. God always yuko pamoja na wale wanaomtafuta. tena mstari wa 19 ndio naupenda zaidi yaani anajua kwamba mateso ya mwenye haki(righteous) ni mengi lakini anamponya nayo yote. ni kweli there many troubles hindering us lakini God will faithfully help us once we truly trust in him.
1Nyakati 5:20 inasema" wakapata msaada juu yao, nao wahajiri walitiwa mikononi mwao na wote waliokuwa pamoja nao, kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani, naye atayatakabali maombi yao kwa sababu walimtumaini. ukisoma english bible tafsiri ya NIV, he answered their prayes because they trusted in him. tunaona tena kuwa Mungu aliwajibu kwa kuwa walimtumaini, where have you being trusting in times of troubles??
Nataka niwakumbushe wandugu na wapendwa katika Bwana kwamba God is so faithful , anaweza kufanya makubwa mno katika maisha yetu lakini ni jukumu langu na lako kuhakikisha tunatembea katika mapenzi yake, tuhakikishe kwamba tunakuwa Righteous all the time!! kuna kipindi nawaambiaga watu kuwa God has principles and thats one of his principle kwamba "serve him well, he serves you well" Barikiwa.....................
STAY INSPIRED!!!!!!
No comments:
Post a Comment