Tuesday, February 23, 2016

SOMO: NJIA TANO ZA KUMJUA MUNGU VIZURI.


BWANA Yesu apewe sifa wandugu............
Inawezekana umeokoka na Yesu anaishi ndani...ila inawezekana pia haujamjua huyu Yesu vizuri........ kudhibitisha haya soma Marko 4:35-41, utaelewa. ukisoma mstari wa 41 unasema" wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, ni nani huyu hata upepo na bahari humtii?
Hapo tunaona kwamba wanafunzi wa yesu walikua nae siku zote, waliona miujiza yake, ishara na maajabu lakini siku ya dhoruba walishangaa kuona upepo na bahari vikimtii.......!!!! kwaiyo hawakumjua Yesu vizur. nimepata mafunuo katika njia za kumjua Mungu vizur.......fuatilia!
1 KUMTAFUTA KWA BIDII
Mithali 8:17 inasema" nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. hapa anasema kuwa anatupenda...inawezekana unampenda Mungu na kwanza sidhani kama kuna mtu ukimuuliza kama anampenda Mungu atakujibu kuwa Hampendi, wote watasema wanampenda ila ukiendelea anasema wanaomtafuta kwa bidii ndio watakao muona. nikagundua kuwa kuna tofauti ya KUMPENDA, KUMTAFUTA na KUMTAFUTA KWA BIDII. inawezekana unampenda na unamtafuta, sasa nataka uweke bidii ili uweze kumwona. Zaburi 105:4 inasema "mtakeni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake sikuzote......sasa hapa bidii iko wapi? ni pale alipomalizia kwa kusema SIKUZOTE! Mithali 13:4 inasema "nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.
2 KUMTAFUTA KWA MOYO WAKO WOTE
Kuna nyimbo tulikua tunaimba inasema" jesus is number one, is everything to me! sijui kama huwa unamaanisha ukiimba hii nyimbo? Yeremia 29:13 inasema" nanyi mtanitafuta na kuniona, mkinitafuta kwa moyo wenu wote" hapa anamaanisha kuwa u give up everything just to have him. kumbuka Mathayo 6:33, sasa watu wanaigeuza hiyo na kuweka mambo yao mengine mbele.
Kumb 4:29 inasema"lakini huko, kama mkimtafuta BWANA Mungu wako utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote. Mathayo 22:37-38 inasema" akawaambia mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili yako yote. ni ngumu wapendwa kumjua Mungu ipasavyo kama bado hatufanyi kama maandiko yasemavyo....Bwana atusaidie!!!!
3 KULIJUA NENO LAKE
mwalimu anapofundisha wanafunzi darasani huwa anawaachia notes wakasome...unajua kwanini? ili walijue lile somo vizuri kama isingekua ivyo basi ingeishia darasani tu na mtiani unakuja. sasa hivyo hivyo, mafundisho kanisani hayatoshi lazima tuwe na muda wa kumtafuta Mungu kupitia maandiko yaani NENO LAKE! Mathayo 22:29 inasema" Yesu akajibu akawaambia, mwapotea kwa kuwa hamjui maandiko wala uweza wa Mungu. inamaana kupotea kwetu inasababishwa na kutokujua neno la Mungu na kwa kulijua neno la Mungu inatusaidia kumjua zaidi na zaidi. Soma Mithali 2:1-5...mstari wa 5 unasema" ndipo utakapo fahamu kumcha Bwana na kupata kumjua Mungu.
4 KUISHI MAISHA MATAKATIFU
Mungu anaheshimu sana watakatifu...sijui kama unajua hilo! soma Zaburi 25:14 inasema" siri ya Bwana iko kwa wale wamchao, na yeye atawajulisha agano lake" sasa unataka nini tena? neno li wazi Mungu ukiwa karibu na Mungu kwa maana ya utakatifu, utamjua Mungu vizuri. ipo mifano ya kina henoko, eliya n.k.
5 KUWA NA ROHO MTAKATIFU
inawezekana ukawa unaishi kumbe roho alishaondokaga zamani, pengine ulijichafua akakuacha maana we ni hekalu lake! Wakorintho 2:10-11 inasema" lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho, maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu. maana ni nani katika binadamu ajuaye mambo ya binadamu ila roho iliyo ndani yake? vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna afahamuye ila Roho wa Mungu.
Wapenzi Mungu awabariki sana kwa kusoma. usidhani utapoteza mda kwa kusoma, na kwa yeyote atakayesoma somo hili nakuombea sasa;
Mungu anaenda kubadilisha maisha yako na hautakuwa kama ulivyokuwa hapo awali........mwenye matatizo yanaondoka katiika jina la Yesu Kristo, mgonjwa unapokea uponyaji wako sasa, umekosa amani Mungu anakupa amani sasa na hakika utaenda kuuona ukuu wa Mungu katika maisha yako...AMEN
STAY INSPIRED!!!

SOMO: JE UNAZO NGUVU ZA MUNGU NDANI YAKO?


Bwana Yesu apewe sifa wandugu..........!
Leo ntaenda kuongelea nguvu za Mungu katika maisha yako.
kama kichwa kinavyosema, inawezekana nguvu za Mungu katika maisha yako hakuna au zimepungua.
Tuanze kwa kusoma Mdo 1:8 inasema " lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajillia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashaidi wangu katika yerusalemu na katika uyahudi wote na samaria na hata mwisho wa dunia" hapo juu nimesema inawezekana huna kabisa nguvu za Mungu au umepungukiwa na hizo nguvu. zipo sababu;
1 HUJAZAZWA ROHO MTAKATIFU
2 ROHO HAYUMO TENA NDANI YAKO
inawezekana umeokoka lakini bado hujajazwa Roho Mtakatifu kwaiyo ni ngumu kuwa na nguvu maana tumesoma pale kwamba mtapokea nguvu akiisha kuja kwenu. pia inawezekana huyu Roho Mtakatifu hayumo tena kwa maana ya kwamba labda ulijichafua kipindi fulani katika maiha yako, ulirudi nyuma naye akakuacha maana wewe ni hekalu lake. na ndio maana tunashauriwa kujazwa maana ziko faida nyingi za kuwa na Roho Mtakatifu.
Sasa tuangalie tena Waefeso 3:20 inasema" basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. kwaiyo kumbe Mungu anafanya kazi kwa kadri ya ngu zilizopo dani yetu!!!! ndio maana yake, sasa jiulize kama wewe huna hizo nguvu za Mungu ndani yako inakuwaje?? kuna umuhimu tena mkubwa sana ya kuwa na nguvu za Mungu ndani yetu. kwaiyo hapa inategemea sasa,
Wafilipi 4:13 inasema" nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu" tunaona tena kumbe tunayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu yaani Roho Mtakatifu. ndio maana nikasema hapo juu iko shida kama huna Roho Mtakatifu na hii imekuwa sababu ya watu wengi kushindwa kiroho yaani kuanguka au kurudi nyuma! andiko linasema tunayaweza mambo yote katika yye atutiaye nguvu, sasa kama huna huyu Roho inakuwaje hapo?
2Tim 4:17 inasema" lakini Bwana alisimama akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu hata wasikie mataifa yote nami nikaokolewa katika kinywa cha simba" paulo anazidi kutuonesha faida za kuwa na nguvu za Mungu ndani yetu.
Nguvu za Mungu ni muhimu sana katika maisha yako mpendwa, kama nilivyosema hapo awali inawezekana hujawahi kujazwa kabisa au Roho Mtakatifu hayumo tena ndani yako. kumbuka Mdo 1:8 kwamba mtapokea nguvu akiisha kuja Roho Mtakatifu katika Maisha yenu. ni ngumu sana kuweza bila kuwa na nguvu za Mungu, wengi wamerudi nyuma, wameanguka maana nguvu za Munngu zenyekuwawezesha hazimo ndani yao kama Wafilipi 4:13.
STAY INSPIRED!!!!!!!!!

SOMO: UKITEMBEA KATIKA MAPENZI YA MUNGU, YEYE ATATIMIZA HAJA YA MOYO WAKO NA KUKUSHINDIA.


Imefika sehemu tumetaka na kutamani baraka kutoka kwa Mungu na kujiuliza mbona mimi sibarikiwi! na pengine tunapokuwa katika shida vivyo hivyo lakini yamkini tukakata tamaa maana tuliona kama hakuna msaada. katika somo hili nataka tujifunze kitu kimoja kwamba ukitembe katika mapenzi yake, yeye ni mwaminifu hata kukufanyia mambo ya ajabu kama Yeremia 33:3 inavyosema.
Isaya 65:24 inasema" na itakuwa ya kwamba kabla hawajaomba nitajibu na wakiwa katika kunena nitasikia" unaona kumbe Mungu anajua haja ya mioyo yetu.......yaani kabla hata hujaomba yeye anajua unachotaka kumwambia. shida inaanzia hapa! wote tunajua kuwa dhambi ni chukizo mbele zake, sasa how do you expect him to have you blessed while unamchukiza???? kuna somo langu linaitwa "TUNAMZUIA MUNGU KUTUBARIKI KWA SABABU YA MAOVU YETU" kama utakuwa utataka kuelewa zaidi waweza kupitia blog yangu victorchubwablogspot.com.
Tusome tena Isaya 66:2b inasema" lakini mtu huyu ndiye ntakayemwangalia mtu monge, mwenye roho iliyopondeka(mnyenyekevu), atetemekaye asikiapo neno langu" tunazidi kuona kuwa kumbe Mungu anajishuguisha zaidi na wale wanaojishugulisha naye. siku hizi watu wamegeuza maandiko kwa mfano Yakobo 4:8 inasema "mkaribieni Mungu naye atawakaribia" sasa siku hizi imekuwa tofauti yaani watu wanataka Mungu ndo awakaribie kwanza.kwaiyo si rahisi kama unategemea kubarikiwa na kuponywa wakati hufanyi yaliyo mapenzi yake.
Zaburi 34:18-19 inasema" Bwana yu karibu na wao waliovunjika moyo na waliopondeka roho huwaokoa, mateso ya mwenye haki ni mengi lakini Bwana humponya nayo yote. napapenda sana hapa....embu jaribu kusoma kwa makini sana jinsi anavyosema. God always yuko pamoja na wale wanaomtafuta. tena mstari wa 19 ndio naupenda zaidi yaani anajua kwamba mateso ya mwenye haki(righteous) ni mengi lakini anamponya nayo yote. ni kweli there many troubles hindering us lakini God will faithfully help us once we truly trust in him.
1Nyakati 5:20 inasema" wakapata msaada juu yao, nao wahajiri walitiwa mikononi mwao na wote waliokuwa pamoja nao, kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani, naye atayatakabali maombi yao kwa sababu walimtumaini. ukisoma english bible tafsiri ya NIV, he answered their prayes because they trusted in him. tunaona tena kuwa Mungu aliwajibu kwa kuwa walimtumaini, where have you being trusting in times of troubles??
Nataka niwakumbushe wandugu na wapendwa katika Bwana kwamba God is so faithful , anaweza kufanya makubwa mno katika maisha yetu lakini ni jukumu langu na lako kuhakikisha tunatembea katika mapenzi yake, tuhakikishe kwamba tunakuwa Righteous all the time!! kuna kipindi nawaambiaga watu kuwa God has principles and thats one of his principle kwamba "serve him well, he serves you well" Barikiwa.....................

STAY INSPIRED!!!!!!

Thursday, February 18, 2016

SOMO; JINSI YA KUWA MTU MZURI/ MWEMA MACHONI PA WATU.


Mwanzo 4:7 inasema" kama ukitenda vyema utapata kibali? usipotenda vyema dhambi iko mlangoni ina kuotea"
Kwaiyo ili ukubalike ni lazima kutenda mema.....hapa Mungu alikuwa akimwambia kaini.........ni dhahiri hata sehemu tunazoishi, unaweza jiuliza"mbona upati kibali kwa wenzako?? mbona unachukiwa?? hapa nimejaribu kukupa mbinu ambazo zitakusaidia kuwa mwema machoni pa watu..............fuatilia!
1 JIFUNZE KUACHILIA/ KUSAMEHE
hakuna kitu kinachomuumiza mtu kama yeye akikukosa alafu wewe ukasamehe na usilipize ubaya kwa ubaya. Petro aliambiwa na Yesu samehe saba mara sabini. siri kubwa ya kukufanya uonekane mwema sio tu kusamehe, na kuachilia pia. kuna msemo unasema "nimekusamehe ila sito kusahau" kumbuka kama na Mungu nae angekua anatumia huo msemo ni dhahiri wengi tungekua tunapokea kichapo kila siku. haijalishi ni adui yako, ndugu yako au mtu yeyote..wewe samehe na mwisho wa siku alie kukosea ataomba msamaha mwenyewe.
2 USIWE MTU WA HASIRA
hii inaweza kuendana na hapo juu, lakini tofauti ni kwamba utakiwi kuwa na hasira za hovyo hovyo hata ktk mambo ya kawaida. biblia inasema" hasira inakaa kifuani mwa mpumbavu" kuna watu wanaopenda kudhila dhila, kukasirika kasirika hata kama amekanyagwa bahati mbaya kwenye daladala basi atakasirika na kutupia maneno mengi na pengine matusi.
3 KUWA MWAMINIFU NA MKWELI
Watu watakupenda sana. mimi nina mifano mingi sana ya jinsi uaminifu ulivyo nisaidia watu kunipenda na kuniamini. hili nimeliona hata kwa wazazi wangu, wametokea kuniamini sana na upendo naona unazidi kiasi cha kwamba nikiomba chochote napewa na napewa ruhusa ya kufanya lolote maana wananiamini kwamba sitawaangusha.
4 WASAIDIE WENGINE
siri kubwa ya kukubalika, ni kusaidia jamii inayokuzunguka. najua mnamjua mohamed dweji, jiulize kwanini watoto wa singida wanampenda sana...ni kwa sababu amejikita kwenye kusaidia na kutoa. juzi mengi amesaidia walemavu na wenye shida usishangae kuona anependwa na kukubalika sana.unaweza usiweze kwenda kwa yatima na wajane lakini jamii tu inayokuzunguka, je unasaidia na kushirikiana nao?
5 WASIKILIZE WENGINE/USHAURI
Kuna watu wanapenda maamuz yao ndiyo yawe final...hawataki kusikiliza wengine. kuna msemo unasema "bora mbili kuliko moja" yanapokuwa mawazo mawili ni bora kuliko la kwako tu.na hii inatokea sana katika mahusiano, mume anapenda kuwa na maamuzi ya kipekeyake bila kumsikiliza mwezake.pia kwa kuwasikiliza wengine unajifunza mengi.
6 JITAMBUE 
Tunaishi katika dunia ambayo kuna watuhawajitambui kabisa. mwengine ana umri mkubwa ila mambo bado ni ya kitoto, kwa nini? ajajitambua! unaojitiambua ni rahisi sana mtu mzuri kwa jamii yako, hakuna apendaye utoto unaofanya hyo itaelekea watu kukudharau na kukuona mjinga. mfano wanaopenda sifa mbele za watu. na siku hizi watu huwa wanakuchekea ila moyoni hawakupendi hata chembe.
7 KUBALI KUSAHISHWA/MAONYO
wapo ambao hawapendi kabisa kuonywa. tambua hii inakusaidia kujua wapi umekosea na ujirekebishe, wengine wanaposaidiwa wanakasirika, namna hii ni ngumu kubadilika. 
8 JIHESHIMU/ HESHIMU WENGINE
dont expect to be respected if u dnt respect ur self. lazima kwanza ujiheshimu ndipo utaheshimiwa. heshimu wengine, siku hizi heshima kidogo kwa vijana ni F, ila hii inasaidia sana unapo heshimu watu wa jamii yako, unakubalika si na wakubwa tu hadi wadogo.
Mungu awabariki sana......tujaribu kufanya haya na nakuhakikishia lazima utakubalika tu maana huko ndiko kutenda Mema.
STAY INSPIRED!!!

SOMO: JINSI YA KUIMARISHA MAHUSIANO AU NDOA YAKO (HOW TO MAKE YOUR RELATIONSHIP OR MARRIAGE STONG)


Shaloom.....natumai mu wazima wa afya. it has been a long time since i last posted my last somo. leo katika mtiririko wangu wa kufundisha, ntaongelea mahusiano. inawezekana una mchumba, either your expecting kuoa au kuolewa au pia kwa wale ambao wako katika ndoa tayari, haya mambo yanaweza kuwa msaada kwako katika kudumisha mahusiano yenu.
1 JENGA UAMINIFU/ KUAMINIANA
Hapa kumekuwa na tatizo sana kwa watu wengi. unaweza ukawa mwaminifu kabisa lakini angalia mambo unayofanya yasije yakaweka mashaka kwa mwenzi wako. mfano simu zimekuwa ni chanzo cha kuondoa uaminifu ktk mahusiano. unakuta hutaki mwenzio aguse kabisa simu yako na pengine ukipigiwa unaenda kupokelea nje au unakata ili uongee badae... labda ni marafiki zako lakini kwa jinsi unavyo jishuku, inaondoa uaminifu kwa mwenzio. na kutokuwa na uaminifu hata ukienda kazini ukachelewa kwa sababu zisizozuilika, mwenzako atajua ulikua nyumba ndogo.
2 SAMEHE HARAKA NA KWELI (ACHILIA)
Hapa unakuta kitu kidogo tu kinazua mbonge la mtafaruku wakati mngesameheana kingeisha mapema. huwa kuna msemo napenda kuutumia na huwa unanisaidiaga, unasema"GIVE UP IF POSSIBLE TO AVOID QUARRELS" tambua quarrels za kila siku zinasababisha mahusiano kuvunjika maana mtachokana haraka.
hii sio rahisi kwa wengi lakini ni vyema ukubali yaishe hata kama mwenzio ndio mgomvi.
3 KUBALI UDHAIFU WAKO/ MAPUNGUFU
it is very obvious that men always hawatakagi kuwa inferior wala kushindwa, ni rahisi kwa mwenzio kukusaidia pale anapotambua udhaifu au mapungufu ulionayo. if u wont admit ur weakness, u will live a hypocrite life ambapo itafika sehemu utashindwa then itapelekea mahusiano kuvunjika.
4 ONYESHA UPENDO WA KWELI
Kama kuna kitu kinatakiwa kiwepo katika mahusiano yoyote basi ni upendo wa kweli. kutokua na upendo wa kweli kunaweza kupelekea mwenzako akahisi kwamba una michepuko, lazima kuonesha upendo wa dhati unless otherwise una mtu mwingine lakini kama yuko peke yake basi huna budi kumwonesha that u real love and care.
5 PEANENI MDA
sio kila saa kila siku ni kuonana mtindo moja,Hapa namaanisha sio kila saa mnataka muwe wote tu.hii inapunguza hali ya kummiss wenzi wako na ndio maana unaweza ukaona kama hakupendi kumbe sababu mpo wote kila mara na hii inapelekea mazoea kwaiyo hamu ya kukumiss inapotea taratibu na badae kuona kawaida.
6 ONGEENI MAMBO YA MSINGI NA KIMAENDELEO
kuna rerationship zingine wanawaza mapenzi tu, wao wakikutana stori ndio hizo...that relationship will neva work coz mnachowaza will neva develop your relatinship....talk about findind a solution to problems, how to overcome obstacles in your relationship let start a business na mengine mengi!
7 KUTOKUELEWANA NI KAWAIDA
Kuna wanaodhani kuwa kila siku ni halelluyah.....hapana mataizo yanakuwepo kwaiyo ni vyema ukajua na kujiandaa lasivyo utasema "werent meant to be together" na utaishia kubadili wapenzi. know that every one has his/her own attitude so make sure you know how to deal with it.
8 HESHIMA/KUHESHIMIANA/KUJIHESHIMU
mnatakiwa kueshimiana......mwanaume usijiwekee kwamba wewe ndo unatakiwa kueshimiwa tu...HAPANA! unatakiwa kumheshimu mwenzako, sikiliza mawazo yake, heshimu maamuzi yake hivyohivyo kwa wanawake. thats how your relationship will become strong.unatakiwa pia utambue kuwa ur in a relationship so respect ur self, angalieni mavazi yenu, yawe ya heshima, usafi wako binafsi.
9 MAWASILIANO
hii pia ni jambo muhimu sana. mfano unakuta mtu anafanya mambo yake bila kumjulisha mwenzake, anaondoka au yupo mahali taarifa hatoi!!!! sasa kwanini usionekane kuwa tatizo katika mahusiano?
10 KUFURAHI PAMOJA
Wengi hawajui, tendo hili linaimarisha sana mahusiano. kuna muda unatakiwa mtoke outing pamoja, mle pamoja mfurahi pamoja. (hii ni kwa wanandoa sana sana ila walio katika mahusiano wawe waangalifu wasije anguka katika dhambi)
Mungu awabariki, ni hayo machache niliyo nayo. ihope u will learn something!
STAY INSPIRED!!!!

Friday, February 5, 2016

SOMO:MBONA UMERUDI NYUMA? JITIE NGUVU, SONGA MBELE.


Wapo watu waliorudi nyuma kwa sababu tofauti tofauti. wengine wamerudi nyuma kwa sababu wamekataa au wamekatishwa tamaa, wengine wamerudi nyuma sababu wanaona kuokoka kwao hakujawa na faida au msaada wowote katika maisha yao. Nataka utambue kitu kimoja mtu wa Mungu, inawezekana wewe ndio chanzo cha kurudi kwako nyuma!! wapendwa wengi leo tumezoa kusema "shetani amejiinua" katika kila jambo. Nataka ujue kuwa unaweza ukawa unamwendekeza shetani.
mfano, kumbuka kile kisa cha yusuph, laiti kama yusuph asingemkimbia mke wa potifa, basi angeanguka katika dhambi ya uzinzi.
Wagalatia 5:7 inasema " Mlikuwa mkipiga mbio vizuri, ni nani aliyewazuia msitii kweli" paulo alikuwa akiwashangaa wagalatia kwamba walikua wakisimama katika imani, sasa ni nini kilikuwa kimewatokea paka wakageuka au wakarudi nyuma. kama nilivyotangulia kusema hapo juu, kuna mwingine anaweza akaonaa kwamba kuokoka hakuna faida yoyote kwake.....kitu kingine wapendwa tunachokosea ni kufikiri kwamba ukisha okoka kila kitu kinanyooka HAPANA! unapookoka shetani hafurahii hata kidogo na unakuwa umetangaza vita na yeye kwaiyo sidhani kama ukiwa vitani huwa mambo yanakuwa mazuri!!! ni lazima kupambana ili uweze kushinda.
Hosea 14:1 inasema"ee israeli mrudie BWANA, Mungu wako maana umeanguka kwa sababu a uovu wako. nilitangulia pia kusema kuwa inawezekana ukawa chazo cha kurudi kkwako nyuma....hapa hosea anawaambia wana waisraeli wamrudie Mungu maana wameanguka kwasababu ya maovu wanayotenda. unajua Biblia inasema usiipende dunia wala mambo yalliyomo ndani yake katika 1 yohana 2:15, huwezi ukasimama wakati unaipenda dunia lazima dunia itakuvuta tu na mwisho wa siku utarudi nyuma.
Wagaltia 1:6 inasema" nastaajabu kwa kuwa mmemwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo na kugeukia injili ya namna nyingine" kuna wengine pia wamerudi nyuma na kugeukia injili ya namna nyingine. kwanza nataka kukwambia kuwa mahali ulipo upo mahali sahihi kabisa. wapo watu kila kukicha wao ni kuhama makanisa pengine wakitafuta miujiza n.k lazima utayumbishwa na upepo tuu. kuna manabii wa uongo hata Biblia inasema sasa kama we ni wa kuhamahama kwanini usinaswe?? na tatizo nililokuja kuligundua ni kwamba wakristo wa leo wanataka sana miujiza ya papo kwa papo. soma Yohana 5:1-9, kisa cha yule mtu ambaye alikuwa hawezi miaka thelathini na minane kwenye birika la Bethzatha. yeye akuwa na mtu wa kumuingiza kwenye birika ila kuna siku yesu alikuja akamkuta palepale na kumponya......ndivyo na wewe itakavyokuwa yesu atakukuta hapohapo na kukuponya huna haja ya kuhangaika, utapishana na muujiza wako bure.
Waebrania 10:31 anashangaa anasema kuwa ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai. ni sawasawa na mtu umeokota dhahabu alafu ukaja ukaitupa kwa sababu huitaki!! watu watakushangaa.......na wokovu ni wathamani sana, hivyo shikilia sana ulicho nacho.
katika ufunuo 2:5 inasema kumbuka ulipo anguka ukatubu, mpendwa kama ulianguka kwa sababu moja wapo ya hizo hapo juu ni vizuri na muda muafaka ukatubu. Mungu anasema nirudieni mimi, kwaiyo yuko radhi leo kukupoke ukirudi.Barikiwa
STAY INSPIRED!!!!!!

Tuesday, February 2, 2016

SOMO: USILALAMIKE, MKUMBUSHE MUNGU, YEYE NI MWAMINIFU ATAFANYA.


Shalom.........
Isaya 43:26 inasema" unikumbushe na tuojiane, eleza mambo yako upate kupewa haki yako" angalia kwa makini sana andiko hili lilivyo na nguvu........hapa Mungu anasema kwamba umkumbushe, muhojiane, ueleze mambo yako alafu upewe haki yako.
Maana ya HAKI ni, kitu au jambo ambalo mtu anastahili kupata. kwaiyo kwa maana nyinine ni kwamba Mungu amesema umkumbushe, muhojiane, ueleze mambo yako uweze kupewa stahili zako.
Je Mungu anasahau mbona anataka umkumbushe? tafsiri ya kingereza "NIV Bible" inasema " reviw the past for me, let us argue the matter together state the case for innocence" Mungu huwa ana kanuni, anataka tutende mema kwanza alafu ndipo na yeye atutendee sisi. ila wanadamu tumegeuza na kumtaka Mungu atutendee wema kwanza. kwa mfano ukisoma Yakobo 4:8 inasema " mkaribieni Mungu naye atawakaribia ninyi" sasa sisi tumegeuza na kutaka yeye ndo atukaribie. Kwaiyo anaposema umkumbushe, anataka umpe sababu za kwanini unataka kutendewa unayoomba.
Na hapo ndipo watu wengi tunapokosea sana, tunataka tupewe haki zetu toka kwa Mungu lakini at the same time sisi atumpi anayotaka, ukisoma Mika 6:8 utaelewa ninachosema. swali linakuja tena, Je unacho cha kumkumbusha Mungu???
Isaya 38:1-5, hii ni habari ya Hezekia. Mungu alimtuma isaya kwenda kumwambia kuwa lazima afe, ila napenda sana ule mstari wa 3, unasema " akasema, ee Bwana kumbuka haya, nakusihi kwamba nimekwenda katika kweli na kwa moyo mkamilifu na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. unaona alichofanya Hezekia ni kwenda kwa Mungu na "STRONG REASON OF WHY HE DOES NOT DESERVE TO DIE YET" Je unacho cha kumkumbusha Mungu kama Hezekia?
Mdo 9:36-43, Hapa tunaona habari za mtu aitwaye Tabitha tafsiri yake ni dorkasi, alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizotoa. alipokufa wale wajane na watu aliowasaidia walihuzunika sana, wakatuma ujumbe kwa Petro. sasa mstari wa 39 unasema" Petro akaondoka akafuatana nao. walipofika wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye wakalia na kuonyesha zile kanzu na nguo alizoshona dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. Mungu alimfufua dorkasi kwa sababu wale wajane walimwonyesha Petro juu ya matendo mema aliyofanya dorkasi naye petro alimkumbusha Mungu.
Inawezekana unalalamika sana majaribu yanapokusonga au unaona Mungu yupo mbali na wewe maana umeomba sana ila bado hujafanikiwa, pengine huna cha kumkumbusha Mungu. kama wewe ni mwaminifu kwa Mungu basi una kila sababu ya kumkumbusha juu ya jambo fulani naye atafanya. Hezekia aliweza kumkumbusha Mungu kwanini wewe ushindwe na umekuwa mwaminifu kwake??
ukisoma Waamuzi 6:13, Gideoni alilamika kwa Mungu akisema " ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo yote haya yametupata??? inawezekana umeshalalamika kama Gideoni lakini kumbe unachotakiwa ni kuacha kulalamika na kumkumbusha Mungu. hebu fikiria kama Hezekia angeanza kulalamika badala ya kumkumbusha Mungu, nini kingetokea??
ni muda mzuri wa kuendelea kuwa waaminifu kwa Mungu ili tuwe na kitu cha kumkumbusha hapo badae........"GOD IS A REASONABLE GOD"
Kama unafatilia masomo yangu unaweza ukanipata pia kwenye blog yangu "victorchubwablogspot.com.
au kwa mawasilino 0715918940........STAY INSPIRED!!!!!!!!!!