Saturday, December 26, 2015

SOMO: TUVUE MIILI YETU, TUKAMVAE YESU.

SHALOM!! Namshukuru Mungu sana sana kwa wingi wa fadhili na neema zake kwetu, hakuna mtu ambae alistahili kuiona siku ya leo. juzi nilikua naangalia taarifa kuna jamaa kakatwa mapanga na kufa palepale, jiulize we ni nani au umempa Mungu nini kwa uhai ulionao? kristmas imepita tunatazamia kuuona mwaka mpya..ambayo ni wiki ijayo tu ila tuendelee kumsihi Mungu atuvushe kwa ushindi.
Leo ntawashirikisha somo kama linavyosomeka hapo juu.....inawezekana ukajiuliza huyu Yesu tunamvaaje? Wengi wetu tuna lundo la nguo ambazo tunavaa na kubadilisha kila siku hakuna anae penda kuvaa nguo ileile siku zote hata kama hana ila anatamani siku awenazo nyingi. sasa ninaposema tuvue miili yetu na tumvae Yesu namaanisha kuacha mambo yakale na kuishi maisha mapya. Nimetoa mfano wa nguo maana ni kitu ambagho kinavaliwa kila siku ila sasa tofauti inakuja kwamba tukishamvaa Yesu, yeye anakua ni vazi la kudumu tofauti na nguo za kawaida hakuna haja ya kuvumvua tena.
Tuangalie katika Waefeso 4:22-24 anasema " Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu. mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu ktk haki na utakatifu wa kweli. maandiko tuliyosoma hapo juu yako wazi sana. kwaiyo tunapofanywa upya, tunapotubu na kuishi maisha matakatifu, tunapookoka ina maana tunavua miili yetu na kumvaa Yesu. wengi wetu leo bado wanang'ang'ania miili yao ya zamani wakati washampokea Yesu kristo. ndugu ni ngumu kushinda dhambi kama tunaishi katika mwili. sasa tumapo mva Yesu ni rahisi sana maana yeye ndo anatushindia yote.
Rum 8:13 inasema "kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. kwaiyo bado tunazidi kuona kwamba miili yetu haiwezi kustahimili dhambi bali tuyafisha mambo ya mwili kwa Roho ambayo ndo sawa na kusema kumvaa Yesu hakika tutaweza.
Pia tukiangalia katika Wagalatia 5:16 inasema" basi enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. neno hapa linasema mwili hunashindana na Roho, kumbuka Yesu alisema katika mathayo kwamba Roho i radhi ila mwili u dhaifu......kwaiyo kwa kumvaa Yesu na kuvua miili yetu ndo kuenenda pamoja na Roho ambae ndo anatusaidia kuweza. sura ya 6:8 anasema " maana yeye apandaye kwa mwili atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. 3:27 inasema "maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo, mmemvaa Kristo. pia Paulo anasema sura ya 2:20 " nimesulubiwa pamoja na Kristo,laakini ni hai, wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu.
Paulo anaendelea katika wafilipi 1:21 anasema" kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.
Kwaiyo wapenzi katika somo hili tunaona kuwa tukiishi katika miili hii pasipo msaada wa Roho ni vigumu kumpendeza Mungu, na huo msaada wa roho unakujaje ni pale tunapo mvaa Yesu kama maandiko yanavyosema
.
Tukiwa tunaelekea mwaka mpya, ni maombi yangu kuwa tuanze sasa na Bwana, tusahau yaliopita ya mwaka 2015.....anasema katika neno lake ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya. kama tumvaa yesu kikwelikweli hakika mwaka 2016 kwako unaenda kuwa wa mafanikio na baraka tele, yale ulioomba mda mrefu yatatimia kwa jna la Yesu!!!!!
Anza 2016 na maisha mapya na hakika utamwona Bwana..........................................
STAY INSIPIRED!!!!!!!!!!!!!!!

Wednesday, December 16, 2015

SOMO: KIJANA NA UCHUMI.


Bwana Yesu asifiwe wapendwa, Natumai mu wazima tena. We thank God for this precious day, na leo ntaenda kufundisha somo juu ya kijana na uchumi.
Kwanza inawezekana haujui au bado hujatambua kwamba kijana ni wa thamani sana mbele za Mungu. sisemi kwamba wengine sio wa thamani au hawana umuhimu kwa Mungu, hapana! nimesema hivyo kwa sababu kuna mambo ambayo yanamfanya kijana kuwa wa muhimu sana
1 kijana ni mwenye nguvu(Mithali 20:29, 1Yoh 1:14)
2 ni wakati wa kujenga foundation/msingi wa maisha(future yako)
3 ni wakati sahihi wa kumtumkia Mungu(Muhubiri 12)
Sasa hizo ni baadhi ya sababu za kujua kwanini wewe ni muhimu sana na shetani anajua hilo pia ndio maana wakati wa ujana huna shida sana maana shetani ana deal sana na vijana.
Nisiendelee sana huko maana hilo pia ni somo lingine kati ya masomo nilionayo, ila tuangalie hili la leo''KIJANA NA UCHUMI''
Vijana wengi tumekua tukipata shida katika eneo la uchumi na mwisho wa siku tunajikuta hatuna kitu kabisa. japo kuna maroho ya umaskini na ufukara yanayo fuatilia watu wa Mungu, lakini zipo circumstance ambazo tunajisababishia sisi wenyewe.
Kuna matatizo yanayowapata wengi hasa katika eneo hili la uchumi mwisho wa siku unajikuta mambo mengi hayaendi na unakata tamaa na kuhisi huna bahati. Wapo wanaoshindwa kuoa, kujikimu ndani ya familia zao, kupata maitaji yao ya kila siku, tatizo kubwa likiwa uchumi mbovu.
Labda tuanze na'' KWANINI MTU ANAPATA PESA LAKINI HAIKAI?
Zipo sababu ambazo hupelekea haya na hili tatizo limetukumba wengi sana, mimi nikiwa mmoja wapo ila namshukuru Mungu alienifunulia haya na ndio maana nakushirikisha ili tujikomboe na wote kufurahia matunda ya pesa zetu
Sababu ya kwanza
1 KUTOKUMUHESHIMU MUNGU KWA MALI NA FEDHA
Mithali 3:9-10 anasema mheshimu Bwana kwa mali yako na kwa malimbuko na mazao yako yote, ndipo ghala zako zitakapo jazwa kwa wingi. Wapendwa embu tafakari hayo maneno hapo, yaani unapomheshimu Mungu kwa mali yeye anakujazi ndio maana yake.
Mathayo 6:19-21, Hagai 1:2-8 Katika maandiko haya swaa zima hapa ni utoaji nikimaanisha sadaka,michango kanisani n.k Mathayo anasema usijiwekee hazina Duniani, kwaiyo tunaona Mungu anataka na anaheshimu unapo mtumikia kwa mali na fedha. ukiangali hiyohiyo mstari wa 31 anasema utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na hayo mengine mtazidishiwa.
Malaki 3:8-10 hapa anaongelea zaka tena kamili sio nusu maana kuna watu wanatoa ndio ila sio kamili, ndugu bora usitoe maana ambaye ajatoa na wewe wa nusu ni sawa tu kumbuka anania na saphira( Mdo 5).
2 KUTAMANI KUISHI MAISHA YANAYOKUZIDI UWEZO
Wapo watu wanaotamani kuishi wakati hali yao ya uchumi hairusu.Labda siku Mungu kakubariki ila tatizo linakuja pale flani au rafiki yako ana simu ya samsung note gear basi na wewe unataka hiyo gear wakati hali ya mfuko wako ni techno mchina...utajikuta unatumia fedha ambazo hukupangilia kununua simu ya gharama kubwa, ndugu ridhika na ulichonacho. Waebrania 13:5 anasema msiwe na tabia ya kupenda fedha muwe radhi na mlivyo nayo. 1Tim 6:6 anasema walakini utauwa pamoja nakuridhika ni faida kubwa.
3 MATUMIZI BILA MALENGO/MIPANGO
Hapa napo panashida sana tu. Wengi hatutumii pesa kwa malengo au mipango. Ndugu unatakiwa kuwa na mipango kwa mfano unaweza ukawa unamuomba mtu pesa kila siku alafu jibu lake ni sina......sio kwamba kila siku yeye hana, hapana! zipo ila zimepangiliwa kwaiyo ya kukupa wewe haipo.Unaweza ukakuta umepokea mshahara..mzuri tu ila kama ujapangilia unaweza ukaisha siku hiyohiyo kwa vijisababu visivyo eleweka mara baby kaja anataka hiki na kile mara mmeenda kula bata mara mmeamua kubadilisha mazingira hata nyumbani hapalaliki siku hiyo...mwingine kwa sababu kapata mshahara atataka watu wajue basi oa zitatembea siku balaaa! alafu mtu akiishiwa anaomba maombi kwa pastor!!!! kua ana pepo la umaskini linamfuatilia kumbe ni kutofahamu.
4 KUMDHULUMU MUNGU
Kumb 16:17 anasema kila mtu na atoe kama Mungu atakavyombariki. kumbuka yule mama mjane alitoa kidogo sana maana ndicho alichokua nacho ila angalia Yesu alivyosema.Je utoavyo sadaka kanisani, michango yako ya ujenzi,injili, mafungu ya kumi, ni kama unavyobarikiwa? jibu unalo moyoni. Mdo 5
Kwaiyo labda kabla ya deliverance na maombezi jichunguze kwanza je katika sababu hizi nilizotaja zinakuhusu na kama zinakuhusu anza leo kujirekebisha na kama bado kuna shida, basi hapo ndio tuanze na maombi maana kama nilivyosema hapo juu kuna maroho ya ufukara na umaskini yanayofuatilia watu.
Mungu na atusaidie sote....STAY INSPIRED!!!

Saturday, December 12, 2015

SOMO: UTAKATIFU NDIO MSINGI WA MAISHA YA MKRISTO.


Bwana Yesu Asifiwe, Namshukuru Mungu kwa nafasi nyingine tena. Napenda kukushikisha tena katika moja ya masomo yangu, kama linavyosomeka hapo juu.
UTANGULIZI
Wengi tunadhani kuwa mtu ukishaokoka ni raha tuu na starehe hadi pale yesu atakapo kuja kuchukua kanisa lake. Waebrania 12:14"tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemwona bwana asipokuwa nao" Kwenda mbinguni ni process yenye stages;
1 KUOKOKA
2KUISHI MAISHA MATAKATIFU, kuokoka peke yake hakutoshi kwa wewe kwenda mbinguni.
Msingi ni nini? kamusi inasema, msingi ni kitako cha nyumba, ambapo nyumba hujengwa au kitu cha mwanzo ambacho ni muhimu kuwepo kabla ya vitu vingine kujengwa juu yake au jambo muhimu. kwaiyo baada ya kuona hiyo maana ya msingi tunaweza tukasema, utakatifu ni jambo muhimu kwa mkristo, Mambo ya walawi 11:44" kwa kuwa mimi ni Bwana wenu takaseni nafsi zenu, basi iweni watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu"
Tuanze kwa kuangalia maandiko machache, Mathayo 7:24-25" basi kila asikiaye hayo maneno yangu, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma zikaipiga nyumba ile isianguke kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba" Tunaona kwamba mkristo anaye ishi maisha matakatifu ana fananishwa na nymba iliyojengwa juu ya mwamba, pata picha umejenga nyumba bila ya msingi alafu mafuriko siku yakaja unafikiri nini kitatokea???? kwaiyo wewe ni nyumba na kama ukiishi maisha ya utakatifu basi umeijenga misingi yako juu ya mwamba.
Mithali 10:25" kisulisuli kikiisha pita asiye na haki hayuko tena, bali mwenye haki ni msingi wa milele. tunaendelea kuona kwamba hata misukosuko yaani majaribu na kama Biblia inavyosema majaribu hayanabudi kuja kwaiyo pamoja na hayo yote mwenye haki atayashinda maana ana msingi wa milele ambao ni utakatifu. ukianglia Zaburi 1:6 anaendelea kusisitiza "kwa kuwa bwana anaijua njia ya wenye haki, bali njia ya wasio haki itapotea"
1 Wakorinto 3:11" maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka isipokuwanni ule uliokwisha kuwekwa, yaani yesu kristo" Hapa tunaona kuwa yesu kristo ndio msingi wa maisha yetu. tukiisha kumpokea kama bwana na mwokozi wa maisha yetu hatuishii hapo na ndio maana paulo anasema tuenende kama inavyoipasa injili ya kristo maana yake tuishi kama yeye( YESU). pia ukiangalia Mithali 16:17 anasema "njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu"
Unajua mara nyingi tunaanguka majaribuni, hatufanikiwi, kwasababu tunaishi maisha ya kuigiza. unakuta mtu ameokoka ila uwezi kumtofautisha na ambae hajaokoka. nilikutana na rafiki yangu ambae nilipomshuudia habari za yesu alikubali ila kuna kitu aliniambia nami nilimpenda sana kwa kuwa mkweli.......alisema anapenda sana kuokoka ila nimpe mda afikirie na afanye maamuzi ya busara ili kama ataamua na aamue moja kwa moja. sio siri yaani yule jamaa alinifurahisha sana na nina hakika kama ataokoka siku basi atatushinda hata sisi tuliotangulia ambao tunasuasua. Biblia inasema ni heri kuwa moto au baridi ila sio vuguvugu.
i argue you brothers....lets live a holy life as its a foundation to our everyday life.

Monday, December 7, 2015

SOMO: UMEPEWA NEEMA ILI UPATE KUTUBU.


Bwana yesu asifiwe, namshukuru sana Mungu kwa matendo yake siku hadi siku, na kwa kuwapa uzima had kuifikia siku ya leo tena.
Ni wakati mwingine katika mwendelezo wa masomo yangu, kama linavyosomeka hapo juu. umepewa neema ili upate kutubu.
Wengi hatutambui umuhimu wa neema tulionayo maishani mwetu, kwanza tuanzae kwa kuangalia nini maana ya toba.
Toba ni badiliko la nia akilini, ambayo matokeo yake yamo katika matendo yaliobadilika kwenye kamusi anasema{ majuto kutokana na maovu uliofanya}. Watu wengi wanafananisha msamaha na toba, ingawa vinauhusiano kwa karibu sana. Msamaha ni tendo la kuomba radhi kwa kosa...... sasa kwa mfano mtu akitaka kuokoka anaongozwa sala ya toba....maana yake ukishaongozwa sala ya toba alafu hakuna badiliko katika maisha yako, hiyo siyo toba ya kweli....
Matendo 26:20" bali kwanza niliwahubiri wale wa dameski na yerusalemu na katika nci yote ya uyahudi, na watu wa mataifa kwamba watubu na kumwelekea Mungu, wakitenda matendo yanayopatana na kutubu kwao"
Tuangalie Luka 3:8" basi toenii matunda yapasayo toba" matunda yapasayo toba maana yake kubadilika. tumeona hapo juu kuwa toba ni badiliko kwaiyo nia ya somo hili ni kwamba wengi wetu ni wakristo, tulishaongozwa sala ya toba ila sasa bado hatuzai matunda yapasayo toba kama luka inavyosema. sasa Mungu ametupa neema ya kuishi, tuliona katika somo la UNAITUMIAJE NEEMA ULIONAYO, ila hatujajua kama hiyo neema tuliopewa ni ili tutubu au tuishi matunda yapasayo toba.
Warumi 2:4-5" au waidharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue wema wa Mungu wakuvuta ili uape kutubu" kwaiyo tunazidi kuona kwamba Mungu anatuvumilia au neema yake bado ipo kwetu ili tuweze kutubu. maana kama nilivyosema katika somo lililopita kwamba , maisha tulionayo tumeazimwa tu, sasa itafika saa Mungu atadai chake. je utakua tayari kumrudishia?
2Petro 3:9" Bwana akawii kutimiza ahadi yake kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee wote waifikilie toba" bado maandiko yako wazi kuwa Mungu kamwe apendi mtu apotee na ndio maana bado neema ipo ili wote sasa tuiifikie ile toba, wapo wanaojisifu juu ya neema walionayo! wewe Bwana acha kabisa........
Wapendwa kuna watu wanaweza kuisi kua ujumbe huu unawahusu ambao wajaokoka! Hapana, maisha tunatoishi hayana tofauti na ambao bado hawajampokea yesu, sasa si hata wao wenyewe si watabaki wanakushangaa tu? maana Biblia inasema utawatambua kwa matendo yao......sasa mpendwa matendo yako hayatokani na kutubu kwako, kwaiyo bila shaka hili somo linakuhusu asilimia mia kabisa.
Ni maombi yangu ifikie kipindi sasa tubadilike na nimekua nikisisitiza sana kwenye masomo yangu maana mda tulio nao ni mchache mno!!!!!! Amani ya Bwana iwe nanyi nyote.....Amina