Sunday, January 31, 2016

SOMO: JIFUNZE KUMUHESHIMU MUNGU KWA MATENDO YAKO.


Shalom watu wa Mungu!
Ni jambo la kawaida kabisa mdogo kumheshimu mkubwa, kama wewe na mimi tunavyo waheshimu wazazi wetu na kama neno lisemavyo "waheshimu baba na mama yako upate kuishi siku nyingi duniani"
Leo ntaongelea tatizo ambalo sisi kama watoto tunalisahau au pengine tumelisahau maishani mwetu na tunaona kila kitu ni sawa tu. Wengi tunajisahau sana na setani amekuwa akitujanjia sana kupitia sehemu hiyo.
Kama somo langu linavyosema, ni kweli tunamheshimu Mungu sana tu ila tatizo linakuja, je hiyo heshima tunayompa ni kwa matendo yetu au ni maneno tu?????
Mathayo 15:8 inasema" watu hawa huniheshimu kwa midomo ila mioyo yao iko mbali nami, nao wananiabudu bure wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya mwanadamu. tunaona hapa inavyosema, kumbe kuna watu wanaomheshimu Mungu kwa midomo tu! ni sawa na unavyo waamkiaga wakubwa zako au wazazi wako ila ukitumwa huendi, ukiambiwa usifanye hiki unafanya lakini asubui ikifika, shikamoo iko palepale................
Isaya 29:13 inasema" Bwana akanena kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao ila mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walichonacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa. kuna siku nilifundisha juu ya kumpendeza Mungu na si mwanadamu. ukiangalia kwa makini katika mstari huu anamalizia anasema "na kicho chao ni maagizo ya mwanadamu" yaani kuna watu wanaonekana wanamheshimu Mungu kwa sababu wanaogopa kusemwa na pengine wachungaji wao au wazazi.
Mithali 3:9 inaema" mheshimu bwana kwa mali yako na kwa malimbuko ya mazao yako yote" mbaya zaidi wachungaji wanapoongelea swala hili, watu tumekuwa tukiona kama vile wako wanajipigia debe ili wapate fedha, LA HASHA! ndugu kwa kufanya hivi ni kumheshimu Mungu kwa matendo. kwanza ni chanzo cha Baraka, endelea kusoma mstari wa 10, alafu utasoma Malaki 3:10 uone kama huwa tunapiga stori. kumbuka anania na safira, walikufa palepale baada ya kuiba sehemu ya kumi ambayo walitakiwa kutoa(ukitoa nusu, usipotoa kabisa, Mungu anakuona mwizi tu)....Mungu ana huruma sana fikiria kama ingekuwa enzi za kina safira wangekufa wangapi leo hii???
sifundishi kutoa zaka ila nasema kwa sababu huko ndiko kumheshimu Mungu kwa matendo!
sifundishi kutoa zaka ila nasema kwa sababu huko ndiko kumheshimu Mungu kwa matendo.
tumalizie kwa kusoma Ezekiel 33:31 inasema" nao huja kwako kama watu wajavyo nao hukaa mbele yako kama watu wangu nao husikia maneno yako wasiyatende maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi. lakini mioyo yao inatafuta faida yao. unaona anavyozidi kusema hapa.....maana yake halisi ni unafiki! maana watu hawa hujifanya kama wanamheshimu Mungu kumbe hakuna kitu ndani yao. ni maombi yangu kuwa, kama ulikua unamheshimu Mungu kwa mdomo tu ni wakati wa kugeuka na kufanaya kwa matendo,
Kumbuka kutomheshimu Mungu kwa matendo, "ni sawa na unavyo waamkiaga wakubwa zako au wazazi wako ila ukitumwa huendi, ukiambiwa usifanye hiki unafanya lakini asubui ikifika, shikamoo iko palepale................
STAY INSPIRED!!!!!!!

Friday, January 29, 2016

SOMO: USIFICHE UTHAMANI ULIONAO.

 SOMO: USIFICHE UTHAMANI ULIONAO.
Bwana apewe sifa.......
Kwanza nataka kila mtu atambue kuwa wewe ni wathamani, ukisoma 2Wakorintho 6:20 inasema "maana mlinunuliwa kwa thamani " anaposema mlinunuliwa kwa thamani, ndugu nataka ujue kuwa ulipookoka ilikuwa ni kitendo cha wewe kununuliwa na Mungu,tena kwa thamani kama alivyotangulia kusema hapo juu.
Kwanza nataka kila mtu atambue kuwa yeye ni wathamani, ukisoma 2Wakorintho 6:20 inasema "maana mlinunuliwa kwa thamani " anaposema mlinunuliwa kwa thamani, ndugu nataka ujue kuwa ulipookoka ilikuwa ni kitendo cha wewe kununuliwa na Mungu, tena kwa thamani kama alivyotangulia kusema hapo juu.
Thamani maana yake ni gharama au ubora wa kitu kutokana na hali na kuhitajika kwake kwa jamii. kwaiyo anavyosema, mlinunuliwa kwa thamani maana yake tuna ubora na tunahitajika kwa jamii inayotuzunguka. Sasa wapo wanaoficha uthamani wao nikiwa na maana ya kwamba wapo ambao wanaogopa kutambulika kama wameokoka. pengine mtu anaogopa labda atachekwa na wenzake, atatengwa na jamii, au wakijua atashindwa kuwa huru maana anataka kuendelea na dhambi. Ndigu tambua kuwa Mungu amekuweka uwe nuru ya mataifa kwaiyo unapojificha ni sawa na kuwasha taa alafu ukaifunika au ukaiweka chini ya pishi.
Matendo 4:13 inasema" basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu wakatambua kuwa walikuwa pamoja na Yesu. Nimeapenda pale anaposema hawakuwa na elimu ila watu walistaajabu maana Roho Mtakatifu aliwapa elimu ya kutosha. Hapa tunaona ujasiri wa Petro na Yohana, wenzetu hawakuona tabu ya wao kuhubiri injili na hata kuwa tayari kufa kwa ajili ya Kristo. Rum 1:16 inasema" kwa maana siionei haya injili kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu.kwaiyo unona ni jinsi gani walikuwa wantambua. sasa hivi imekuwa ni shida hata kwa mkristo kwenda kushuudia maana hana ujasiri kwasababu atachoenda kuwakataza wenzake ndicho afanyacho.
2Tim 2:12 inasema" kama tukistahimili tutamiliki pamoja naye, kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi. mfano mzuri ukisoma Mathayo 26:69-79 utaona jinsi petro alivyo mkana Yesu mara tatu, ila ana heri maana iliomba msamaha palepale! unaweza ukawa umemkana yesu tayari, unaokuwa chuoni kwako, maeneo ya nyumbani na hutaki watu wajue umeokoka,huakondiko kumkana, katika Mathayo, Petro akutaka ajulikane kwasababu aliogopa kufa pamoja na Bwana wake! pengine na wewe leo unaogopa kujulikana kwa sababu rafiki zako watakukimbia, au jamii inayokuzunguka itakutenga........SIKIA! ukisoma Luka 9:26 inasema "kwa sababu kila atakaye nionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa Malaika watakatifu. 12:9 inasema "na mwenye kunikana mbele ya watu huyo atakanwa mbele ya Malaika wa Mungu. uunapoona haya kwa sababu nilizotaja hapo juu, tambua hiyo ndiyo haya atakayo kuonea Yesu kristo mbele za Mungu. katika Mathayo 10:32 inasema"basi, kila mtu atakayenikiri mbele za watu, nami nitamkiri mbele za baba yangu. kwaiyo ndugu zangu, tubadilike, aiwezekani tunataka watu waokoke, waje kwa Yesu wakati sisi hatutaki kubadilika.......dont expect changes to others kama wewe mwenyewe ujabadilika.
STAY INSPIRED!!!!!!

Friday, January 22, 2016

SOMO: BADILIKA ILI UBADILISHE WENGINE.


Bwana asifiwe watu wa Mungu!
badiliko maana yake hali inayokuweko baada ya kutokea mageuzo fulani........
Katika somo hili, kubadilika kwa watu kunatokana na maisha yetu kwa asilimia kubwa sana,tunapowashuudia watu tunatamani waachane na dhambi kisha waokoke na kuja makanisani mwetu...lakini tunasahau kwamba inawezekana sisi tukawa ndio chanzo cha wao kutokuokok, mfano wewe labda una rafiki yako hajaokoka, na we umeokoka na unaishi maisha yanayompendeza Mungu, unapomshuudia habari za yesu ni rahisi kwake kubadilika maana anacho kiona ndani yako na unachosema vina uhusiano. ila pata picha wote mnazitungua dhambi kama kawaida alafu unamwambia abadilike, atabaki anakushangaa tu!
Mdo 13:47 inasema "kwasababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, nimekuweka uwe nuru ya mataifa upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia. Tafkari maneno haya kwa umakini mkubwa sana. Mungu anasema ametuweka tuwe nuru kwa mataifa ina maana kile tufanyacho kiwe chanzo cha mabadiliko kwa wasiomjua Mungu. ndio maana ya kuwa nuru yaani matendo yetu mema yawaangaazie mataifa ili kufikia wokovu ndio maana anamalizia na kusema "upate kuwa woovu hata mwisho wa dunia. hapo juu nimesema tunatamani sana kuona watu wanaokoka na pengine tunashuudiaga mitaani mwetu ila tunasahau kwamba maisha yetu yana impact(matokeo) kwa wasiomjua Mungu.kama we ni muhuni usishangae wao kuwa wahuni. lazima uwe kielelezo ili yule unayemshuudia avutike.
Tito 2:6-7 inasema " vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi 7 katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na astahivu. mfano mimi ninaye wafundisha haya kila siku lazima kwanza niwe kielelezo kwenu nyie ili kusudi muamini kile nisemacho. ni mgumu kumwambia mtu abadilike wakati wewe hujabadilika. hapa Paulo alikua anamwambia Tito kuwa awaonye vijana lakini kama hiyo haitoshi yeye kwanza awe mfano kwao.
Isaya 46:6 inasema" naam asema hivi ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za yakobo na kuwarejeza watu waisraeli waliohifadhiwa, zaidi ya hayo ntakutoa uwe nuru ya mataifa upate kuwa wokovu wangu hata mwisho wa dunia.
Luka 2:32 inasema" nuru ya kuwa mwangaza wa mataifa na kuwa utukufu wa watu wako waisraeli. bado anasisitiza kuwa nuru ya mataifa lakini kama nilivyosema huwezi nuru wakati we ni giza! mfano tube light ni nyeupe na ukiwasha mwanga unakuwa mweupe kadhalika kwa zile za bluu, njano na mwanga wake unakuwa hivyohivyo. sasa pata picha ikiwa nyeusi.......................
mwenye masikio na asikie Roho asema na kanisa...AMINA
STAY INSPIRED!!!!!!!!!!

Wednesday, January 20, 2016

SOMO: USIFURAHIE KUSHINDWA KWA MWENZAKO.


Shalom people of God...............!
Sidhani kama mko njiani na rafiki yako mnatembea alafu gafla rafiki yako akateleza kwenye matope na kuanguka chini alafu ukaanza kumcheka badalaa ya kumpa pole na kumsaidia kunyanyuka! sidhani. na wala sijawai kuona katika maisha yangu.
wapo watu leo wanafurahia kuanguka au kushindwa kwa wenzao. yawezekana ni chuoni,matokeo yametoka ukasikia mwenzako ana supplementary au kadisco, kwako inakuwa sherehe. au kanisani au mahali mnapoishi. upo masemo usemao leo kwangu kesho kwako!! waswahili wamesema ila kiukweli kauli hii au msemo huu una ukweli ndani yake kabisa.
Mika 7:8 inasema" usifurai juu yangu, ee adui yangu. niangukapo nitasimama tena nikaapo gizani bwana atakua nuru kwangu" namshukuru dada yangu Upendo nkone aliimba nyimbo hii na pengine unaipenda sana lakini hufuati yale yalioimbwa kwa maana bado unafurai juu ya kushindwa kwa mwenzako. hapa mika anasema usifurai juu yangu, maana nitasimama tena. leo hii jambo hili limekuwa hodari sana,waswahili wamesema tena si kila akuchekeaye ni rafiki yako! inawezekana unacheka na mwenzako, mnapiga stori na inawezekana mwenzako anajua unampenda kupita maelezo maana unamwonesha hivyo, lakini moyoni bado unataka na unatamani ashindwe, bado unamnenea mabaya.
kuna watu hawapendi mafanikio yako na wanakesha wakiomba ushindwe. unaweza ukawa shaidi wa hili ninalosema maana tunaona hata kwenye maigizo, kuna watu wanaenda kwa waganga kulogana au hata kuuana kisa kwanini amemzidi mafanikio. ndugu huyu Mungu tunayemwabudu hana Roho mbaya kiasi hicho! iweje sisi?
Wagalatia 6:1 inasema"ndugu zangu mtu akighafilika katika kosa lolote ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole ukiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. kugafilika ni kuwa katika hali ya kusahau au kupitiwa. paulo anaawambia wagalatia kuwa mtu akijisahau au kupitiwa kwa kosa lolote nyie mrejezeni. hapo juu nimesema inawezekana kanisani kuna wanaofurai kuona fulani amesimamishwa huduma kisa amefanya dhambi ya uzinzi. na pengine ulikuwa unamwona kwamba hali yake ya kiroho inashuka, je ulichukua hatua gani kumrejeza? watu siku hizi tuko tayari kumuacha mwenzetu apotee, na hiyo ni sababu ya kutokuwa na upendo ndani yetu. nilianza kwa mfano pale juu kwamba unaweza ukamwacha nakumcheka rafiki yako aliye anguka kwenye matope njiani?
Yakobo 5:19-20 inasema " ndugu zanngu ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli na mtu mwingine akamrejeza 20 jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke ktk njia ya upotevu ataokoa roho na mauti na kufunika wingi wa dhambi.
Naupenda sana mstari wa 20 yaani anasema utakuwa umeokoa roho na mauti na kufunika wingi wa dhambi. kwaiyo unapowarudisha wenzako kundini anasema umeokoa roho na kufunika wingi wa dhambi. sasa tatizo linakuja sisi wala hatujali inawezekana una rafiki yako unaona kabisa anapotea hayuko katika njia, wewe ndio kwanza hata ujali tena unasubiri kuona mwisho wake! wapo watu wenzao wakishashindwa utasikia "mi nilijua tu lazima yangetokea haya" Ndugu kama ulijua ulikuwa wappi kumuonya?? umesubiri mambo yaaribike ndio useme?
Usifurahie kushindwa kwa mwenzako, unaapo ona mambo hayaendi sawa kaa naye, jaribuni kuyaweka vizuri kama maandiko yanavyosema ktk yakobo na wagalatia.jua kwamba linalompata mwenzako leo nani ajuaye laweza kukupata kesho!
STAY INSPIRED!!!!!!!

Tuesday, January 19, 2016

SOMO: UTAMWENDEA YESU KWA MASHAKA HATA LINI?


Bwana yesu apewe sifa....natumai mu wazima wa afya.
shaka ni nini? hali ya kujawa na wasiwasi na kukosa uhakika wa jambo. hiyo ndo maana ya shaka yaani una kuwa na wasiwasi, huna uwakika na kile ufanyacho.
wengi leo tunamwendea Yesu wetu kwa mashaka na ndio maana hatufanikiwi, hatujibiwi maombi kwa sababu hatuna uwakika na kile tunachokiomba tumejawa wasawasi. pengine unayo imani ndio lakini ni ndogo. ukisoma biblia ya kingereza tafsiri ya NIV inasema" you with little faith"!
Math 18:22-31 Yesu aliwaambia wanafunzi wake wavuke watangulie ng'ambo, huku yeye akibaki kuomba. wakati wanafunzi wamefika katikati, kukkawa na dhoruba kali. ndipo Yesu aliwaendea akienda kwa migu juu ya bahari. wanafunzi walipomwona akitembea juu ya maji wakadhani ni kivuli wakaingiwa na hofu. sasa point yangu inakuja mstari wa 28 "Petro akamjibu akisema Bwana ikiwa ni wewe niamuru nije kwako juu ya maji 29, akasema njoo, Petro akashuka chomboni akaenda kwa miguu juu ya maji ili kumwendea yesu 30, lakini alipouona upepo akaogopa akaanza kuzama! akapiga yowe akisema Bwana niokoe. Mara Yesu akaunyosha mkono wake akamshika, akamwambia ewe mwenye imani haba mbona uliona shaka?
Unaona Petro alipouona upepo aliogopa akaanza kuzaama. kwaiyo alipoogopa tu ndipo alipoanza kuzama ina maana Yesu alivyomwita hakuzama bali alianza kuzama pale alipoona shaka.
Thats how things are today pipo! inawezekana vitu vyako haviendi sawa, haufanikiwi, umeomba lakini hakuna majibu, tambua ya kwamba ulifanya kwa mashaka. Petro alianza kuzama alipoona shaka. alitamani na ndio maana akamuomba Yesu ili nayeye atembee juu ya maji lakini alipoona shaka biblia inasema akaanza kuzama. Yesu yuko tayari kukusaidia ila tatizo unaona shaka!
Yakobo 1:6 inasema " ila na aombe kwa imani pasipo shaka yoyote, maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku." angalia mtu mwenye shaka alivyofananiswa hapa, anasema ni kama wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku. Mungu anataka tuwe na imaani tumuombapo. Yohana inasema nanyi mkiomba lolote kwa jina langu aminini kwamba yatakuwa yenu. hakusema kwamba msubiri yatakuwa yenu hapana! anasema amini tu.
unajua kuna muda huwa nawashangaa watu, wanaona kama miujiza haiwezekani sikatai kuwa kuna watu wana fuataga nguvu za uponyaji nigeria.......ila kwa udogo wa imani yako inafika kipindi huamini kabisa miujiza. tusome Marko 11:23 inasema" amini nawaambia yeyote atakayeuambia mlima(pepo) huu ng'oka ukatupwe baharini wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia yatakuwa yake. sasa unataka nini tena hapo wakati maandiko yako wazi kwamba unao uwezo wa kuamisha milima yaani kukemea pepo na zikatoka ila amesisitiza kuwa usione shaka!
kwaiyo saa nyingine tatizo liko kwako mwenyewe kumbuka pale juu tuliona tatizo lilikuwa la petro maana alianza vizuri ila kwa sababu aliona shaka moyoni mwake ndio maana alimaliza vibaya. vivyo hivyo na wewe yamkini unamwendea yesu kwa mashaka kama petro, na ndio maana tatizo ulilo nalo limekuwa sugu, unataka uponyaji ila una mashaka, wasisi unahisi kama Mungu awezi kukuponya. kumbuka yule mama alietokwa na damu miaka kumi na miwili laiti kama angeona shaka wakati anagusa pindo la vazi la Yesu yamkini hadi leo angekuwa anataabika na ugomjwa wake ila kwa kuwa aliamini toka moyoni, basi pindo tu liliweza kumponya........
STAY INSPIRED!!!!!!!

Sunday, January 17, 2016

SOMO:USIPO BOMOA MSINGI WA DHAMBI ULIOUJENGENGA, UTAENDELEA KUKUTAFUNA.


Kama umeshaokoka na unaendelea kutenda yale uliokua unatenda tambua ya kwamba unaendelea kushindilia msingi wa dhambi badala ya kubomoa na ndio maana ni rahisi kuvamiwa.
2Petro 2:20 inasema "kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na mwokozi Yesu kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Hapa tunaambiwa kuwa wale waliokimbia machafu ya dunia kwa maana ya kwamba mimi na wewe tuliogeuka tukaacha dhambi na kuokoka anasema kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho hua mbaya zaidi........
kichwa cha somo langu ni usipo bomoa msingi wa dhambi ulioujenga, utaendelea kukutafuna! ni kweli tunapoachana na mambo ya dunia tutambue kuwa shetani hafurahii kabisa na ndio maana mtu anapookoka kuna kuwa na upinzani wa mambo ya kiroho zaidi maana shetani yuko kuhakikisha kuwa unashindwa tu. sasa tulipokua upande wa ulimwengu yaani shetani kuna dhambi ambazo tulizoelea kuzifanya mfano mtu alikua mlevi wa pombe tena wakupindukia, sasa anapookoka na kuachana na ulevi, lile pepo la ulevi likimtoka haliendi mbali bado linaendelea kumnyemelea na ndio maana ni rahisi kwa wachanga kiroho yaani waliokoka karibuni kurudi kule walipotoka, kwanini? kwa sababu mapepo bado wananyemelea kilicho kuwa chao..
Nakumbuka kuna dada fulani alifundisha kuhusu kuvunja maagano na laana uliyoweka na shetani...unaweza ukashangaa ni maagano gani ulioweka mfano ulipokua hujaokoka kutoa mimba ilikua kawaida, unapookoka na kuolewa unaweza ukashangaa unakua tasa(sio kwamba mtu akiwa tasa hii ndo sababu hapana) sasa huo utasa unaweza ukasababishwa na wale mapepo maana ulipokuwa kwao ulikua unatoa mimba sasa baada ya kubadilika wanaamua kukufunga tumbo lako!
Luka 11:24-26 inasema " pepo mchafu amtokapo mtu hupitia mahali pasipo maji akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona husema nitarudi nyumba yangu niliyotoka, hata afikapo akiona imefagiliwa na kupambwa ndipo huenda akachukua pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe wakaingia na kukaa humo na mtu huyo hali yake ya kwanza huwa mbaya kuliko ya kwanza. nadhani unaweza ukapata mwanga juu ya kile ninachoongea. kwaiyo pepo anapomtoka mtu, huwa haendi mbali anaendelea kunyemelea kilicho kuwa chake na ndipo maandiko tuliyosoma yanasema akikuta imefagiliwa na kupambwa huenda akachukua wengine saba tena wabaya kuliko yeye alafu anamalizia anasema hali yake ya kwanza huwa mbaya zaidi kuliko ya kwanza..........kwaiyo mpendwa wewe unaweza ukaona ni kawaida tu na pengine ukashangaa kwanini mtu anaanguka katika dhambi tena kirahisi sana, ni kwa sababu hajabomoa msingi wa dhambi alioujenga na kujiwekea ulinzi wa kutosha.
katika Yohana 5:14 inasema "baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu akamwambia, angalia umekuwa mzima usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi.....kwaiyo Yesu alijua kwamba kama mtu yule ataendelea kutenda dhambi ni dhahiri wale mapepo watarudi tu.
Joshua 7:12 Mungu alimwambia joshua kuwa hatakuwa pamoja na wana waisrael kama wasipokiharibu kile walichokuwa nacho kilichoweka wakfu. Ukisoma sura yote ya 7 utagundua kuwa ile dhambi ya wizi iliyofanywa na wana israel kwa kuiba vvile vitu ndo ilikua inaendelea kuwatafuna na ndio maana walikua wakipigwa kila wanapoenda vitani. mstari wa 11 Mungu anawmambia Joshua kuwa asisumbuke kulia kwa sababu israeli wametenda dhambi. ila ukiendelea utaona kuwa baada ya kuharibu kile walichokiiba Mungu alikua pamoja nao na waliendelea kushinda vitani.
kwaiyo tusipobomoa yale tuliyoyaacha na kuendelea kuyatenda yataendelea kututafuna.
STAY INSPIRED!!!!!!!

Saturday, January 16, 2016

SOMO: TAFUTA KUMPENDEZA MUNGU NA SI MWANADAMU.


Praise the living God.........! inawezekana kweli umeokoka, uko vizuri kiimani lakini ukawa unampendeza mwanadamu badala ya Mungu wako.....fuatilia mtiririko huu utaelewa.
katika Wagalatia1:10 " maana, sasa je! ni mwanadamu ninao washawishi, au Mungu? au nataka kuwapendeza wanadamu? kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
haya ni maneno ya Paulo kwa wagalatia. unaweza ukaona ni kwa jinsi gani mtume Paulo alitambua kazi aifanyayo ni kumpendeza Mungu na si mwanadamu. wengi wetu leo tunawapendeza wanadamu wenzetu na si Mungu. mfano wapo watu ambao wanaenda kanisani kwa kuhofia kwamba mchungaji atamuuliza au mshirika mwenzake atamuuliza. yaani ile dhamira yake ya kufanya kazi ya Mungu haitoki moyoni bali anafanya ili aonekane machoni pa watu tu!
kuna ule mfano niliutoa wa rafiki yangu alieogopa kuja kanisani kuokoka ili nikunirishisha. mi nasema ana heri yule jamaa maana anatambua ya kwamba haifaidii kitu mimi kufurai kwa kuwa ntaona kuwa amebadilika lakini moyoni mwake ni tofauti. ndio maisha ya wakristo wengi siku za leo, anaendaa kanisani ili baba yake au mama yake afurai tu au ili mshirika mwenzake afuraishwe pia. na kuna wanaogopa kuwa wataulizwa maswali na mchungaji wao. si washirika tu, wapo wachungaji wanao wanyenyekea washirika kwa mfano unakuta kuna msirika anatoa sana katika ujenzi, michango, anamsaidia labda kusomesha watoto wa mchungaji, anamtegemeza sana mchungaji n.k sasa unakuta mchungaji anaaza kumnyekekea kiasi cha kwamba hata yule mshirika akikosea ni ngumu kwa mchungaji kumwadhibu. mwisho wa siku yule mchungaji anaanza kuweka hofu kwa mshirika wake badala ya Mungu. sababu kubwa ya watu kuwapendeza wanadamu pengine ni kutomjua Mungu vizuri.
1 Thess 2:4 inasema" bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana injili, ndivyo tunenavyo si kama wapendezao wanadamu bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu"( amana ni kitu anachopewa mtu na mtu mwingine ili amtunzie au amwekee, akiba, kitu cha thamani kubwa) Paulo anajaribu kutueleza tena kuwa tumpendeze Mungu anaetupima mioyo yetu. kumpendeza mwanadamu kuna mwisho wake ni sawasawa mtu anaye mtegemea mwanadamu labda watoto walikua wanamtegemea baba sasa amefariki pata picha shida watakayo ipata wale watoto.
Mathayo 6:1 inasema" angalieni msifanye wema machoni pa watu kusudi mtazamwe na wao kwa maan mkifanya kama hayo hampati thawabu kwa baba yenu aliye mbinguni. mstari huu ananifurahisha sana maana anasema hampati thawabu mbele za Mungu. pale juu nilitangulia kusema kwamba inawezekana umeokoka vizuri na ukajua unaenda mbinguni ila bado kikwazo kikawa ndio hiki cha kumpendeza mwanadamu. Yesu aliwaambia waangalie au unaweza sema kwa lugha nyingine jihadharini msije mkafanya wema machoni pa watu. na ndivyo ilivyo leo kwamba mtu anataka asifike kuwa alitoa kiaisi kadhaa kanisani kwenye mchango wa ujenzi ila dhamira yake siyo tumtolea Mungu bali apate sifa kuwa anazo! utasikia mi nimefanya hiki, nimefanya kile kwa kanisa langu tena niliweka bati lote peke yangu, au mtu anasaidia yatima, wajane, wenye shida ili watu wauone wema wake kumbuka kuwa huko ndiko kumpendeza mwanadamu na si Mungu.
mstari wa23:5 inasema" tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu kwa kuwa hupanua hirizi zao huongeza matavua yao. yaani yote hii ni kwamba mtu anafanya ili aonekane tu......na watu wa leo walivyo huwa wanasubiri watu wote wawepo ili aonekane kabisa wala hawezi fanya pekeyake pekeyake.
Kwaiyo wapendwa embu tutafute kumpendeza Mungu, tufike seheme na sisi tuwe kama mtume Paulo aliyetambua kuwa kazi yake si ya kumpendeza mwanadamu.....BARIKIWA!
STAY INSPIRED!!!!!!!

Thursday, January 14, 2016

SOMO: MSIMAMO WAKO KWA MUNGU UKO WAPI?


Yesu asifiwe wapendwa....
Labda kwa kuanza, tuangalie nini maana ya msimamo. katika kamusi ya sasa inasema msimamo ni mawazo ya mtu yenye kuonesha mtazamo wake kuhusu jambo au tendo la kufuata kanuni fulani za maisha.
Baada ya kuona nini maana ya msimamo, pengine tutakua tumeshajua msimamo ni nini!
Msimamo kwa kingereza unaweza ukasema principles.....i believe everyone of us have his or her own principles in life, kama huna thats a shame na tambua unaishi ili mradi maisha yaende tu. Msimamo ni kitu kimoja cha muhimu sana katika maisha, mfano katika mahusiano wengi wetu wanapenda kujua principles za wenzi wao. sasa kwanini msimamo?? msimamo unakusaidia kujiendesha kimaisha. mtu anaejiendesha bila msimamo ni rahisi sana kufanya makosa au kutofanikiwa. mfano kwa wadada ambao wanatongozwa tongozwa ovyo na wakaka, kama hana msimamo wake binafsi ni rahisi kumkubali kila mtu alafu mwisho wa siku kujilaumu.....au kwa mfanya biashara kama hakuna msimamo wa nini ufanye ili ufanikiwe unaweza ukashawishiwa na wenzako na kujikuta kila siku unabadilisha biashara na hakuna mafanikio.
Sasa nikienda kwa upande wa kiroho, kama kichwa cha habari kinavyosema, wengi wetu hatuna msimamo na ndio maana inakuwa rahisi sana kwa mwamini kuanguka au kurudi nyuma.yakitokea mabaya tena yuko tayari hata kumkana yesu kama petro... ili tu asipate tabu au asidhurike. tena wengine wakienda mikoani ndio huwezi tambua hata kama wameokoka. anakuwa kinyonga ghafla!!
kuna pasta fulani alikua na kanisa kubwa tu...hakupendezwa sana na waumini wake maana walikuwa hawapo serious na ibada mara leo waje kesho wasije. siku pasta akamwalika pasta mwenzake ila akamuomba kuwa akija aje kama gaidi,avamie kanisa na kuua wale wanaompenda Mungu.
ilipofika jumapili, wakati ibada inaendelea mara yule pasta akavamia kanisa mkononi akiwa na bunduki.....watu waliogopa sana! yule pasta alisema wote wanaompenda Mungu wasogee mbele huku mikono ikiwa juu, alivyomaliza kukoki bunduki tu, hakukua na mtu kanisani kasoro pasta, wote walikimbia.
huo ni mfano wa kwamba watu wale hawakua na msimamo juu ya Mungu wanae mwabudu. je ingetokea leo ungebaki?????
Danieli 1:1-30, mstari ni mingi sana sitaiandika ila naomba ukasome na uone jinsi watu hawa wa Mungu walivyokua na msimamo mbele za Mungu. wote tunaijua hii stor vizuri sana ila naomba ukasme kwa umakini sana. nawapenda hawa watu sana maana ukisoma mstari wa 16 inasema" ndipo shadracka meshaki na abednego wakajibu wakamwambia mfalme, ee nebukadreza hamna haja kukujibu katika neno hili 17, kama ni hivyo Mungu wetu tunaemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto naye atatuokoa na mkono wako. 18, bali kama si hivyo ujue ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.
hivi embu tafakari maneno ya hawa watu wa Mungu alafu jiulize mimi na wewe tungeweza kweli???? yaani hawa jamaa walikuwa tayari kwa lolote lile ambalo lingekuja mbele yao. labda nikufumbue macho unapokuwa na msimamo mbele za Mungu yeye akuachi. angalia mstari wa 24, ndipo nebukadreza akastaajabu akainuka kwa haraka akanena akawaambia mawaziri wake je! hatukutupa watu watatu hali wamefungwa katikati ya moto? wakajibu wakamwambia, mfalme kweli.
Mungu awezi kukuacha uaibike kamwe! Msimamo wa watumishi hawa ulibadili hata utaratibu wa nchi...kitu cha ajabu sana!
Ni rahisi sana kwa wapendwa kusema wameokoka na wanampenda Yesu lakini hawana misimamo mbele za Mungu. Petro alimwambia Yesu kuwa yuko tayari hata kufa nae ila badae baada ya petro kuona shuhuli ni nzito alimkana mara tatu ila heri yake yeye ambaye alitubu palepale.
msimamo unakusaidia kuishi maisha yanayompendeza Mungu...................
STAY INSPIRED!!!!

Tuesday, January 12, 2016

SOMO: TUMECHAGULIWA ILI TUFANYIKE WANA WA PENDO LAKE.


Shalooom! hope everybody's fine na mwaendelea vizuri...sifa na utukufu ni kwake
Leo tutaenda kujifunza somo kama linavyosomeka hapo juu. Nataka utambue kuwa tumechaguliwa kwa kusudi maalumu na ndio maana nilkalipa somo langu kichwa cha habari kwamba tumechaguliwa ili tufanyike wana wa pendo lake.
KWANINI TUMECHAGULIWA?? kabla ya kumpokea yesu naamini tulishuudiwa ama tulisikia habari za kuokoka na ndipo labda ulipochukua hatua, sasa kile kitendo cha kuchukua hatua yaani kuokoka ndio kuchaguliwa kwenyewe!! angalia Yohana 1:12 inasema " bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu ndio wale waliaminio jina lake......Biblia ya kingereza tafsiri ya NIV inasema"he gave them the right to be become children" tunaona kuwa ukisha okoka moja kwa moja tayari unakuwa ni mwana wa Mungu.
1 Yohana 3:1 inasema " tazameni pendo la namna gani alilotupa Baba kwamba tuitwe wana wa Mungu na ndivyo tulivyo. tunaona makusudi ya Mungu kutuokoa. anaposema pendo alilotupa Baba kwamba tuitwe Wana wa Mungu ni kwamba alituokoa ili tuingie katika ufalme wake yaani tuwe wana wake. kama mtu wa Mungu unatakiwa kutambua kuwa umetengwa au umechaguiwa. kitendo cha kuokoka ni kuchaguliwa yaani imediately unapokua umeokoka jina lako linafutwa katika kitabu cha kuzimu na kuandikwa katika kitabu cha uzima, huko ndo kuchaguliwa!
Wakolosai 1:13 inasema "naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katia ufalme wa Mwana wa pendo lake. embu tafakari maneno haya;
hatua ya kwanza aliyoifanya Mungu ni kutuokoa, wengi tulikua dhambini, watumwa wa dunia kwaiyo alichokifanya Mungu ni kukutoa katika nguvu za giza na kukuleta kwake na ndio maana kwa mfano tunapowashuudia watu ili waokoke au mtu anapookoka anakua amevutwa na Mungu kutoka kwenye nguvu za giza.
hatua ya pili akatuamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake. unaweza ukajiuliza kwanini nimesema kuna hatua ambazo Mungu alifanya! lengo au kusudi la Mungu kutuokoa ni kutuingiza katika ufalme wake kwaiyo yeye akiisha kutuokoa kazi ya pili ni juhudi zetu ni kuhakikisha kwamba tunateka ufalme wa Mungu..sikia, Mathayo 11:12 inasema" Tangu siku za yohana mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu nao wenye nguvu wauteka. kwa mstari huu nadhani utakua umeelewa kwamba iko kazi ya ziada kuuteka ufalme wa Mungu.
Sasa tuangalie kwa karibu hii hatua ya pili.2 Wakorinto 6:17 inasema "tokeni kati yao mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kilicho kichafu, nami nitawakaribisha. kama nilivyosema Baada ya hatua ya pili ambayo ni kukuhamisha na kutuingiza katika ufalme wake, 2 Wakorinto 6:17 inatuambia cha kufanya sasa hili tuuteke au tuingie katika ufalme wake. kile kipengele cha mwisho anasema nami ntawakaribisha, sasa atatukaribisha wapi??? ina maana ndio atatukaribisha katika huo ufalme. na ni baada ya kupambana kama tulivyosoma katika Mathayo 11:12.
Usifikiri kwamba tukiisha okolewa moja kwa moja ni Raha tu hapana!! iko gharama sasa ambayo ndo inatupeleka katika ufalme wake.
Warumi 8:29 inasema" maana wale aliowachagua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndigu wengi. kwaiyo tatizo linakuja au unaweza ukajiuliza kama Mungu alituchagua kwanini tunashindwa na ibilisi???? Mpendwa, watu wengi wanashindwa kutambua kuwa ukisha okoka umechaguliwa kwaiyo hakuna kurudi ulipotoka ndio narudi katika ile hatua ya pili ya kuuteka ufalme wake....sasa usipoelewa kuwa umechaguliwa kwa makusudi , huwezi au ni ngumu kusonga mbele. mfano ni pale labda mwanafunzi anapochaguliwa kujiunga na sekondari, au labda umefaulu form 4 ukachaguliwa....ukishaenda shule uliochaguliwa si jukumu tena la necta au wizara ya elimu iliyokuchagua kuja kukusomea ili ufaulu au likupitishe tena katika hatua ifuatayo..hapana! ni juhudi zako.
STAY INSPIRED!!!

Sunday, January 10, 2016

SOMO: DHAMBI NI KIKWAZO CHA UPONYAJI.


Shaloom!!!!
katika somo hili, nimegundua kuwa dhambi imekua chanzo cha mambo kuharibika ktk maisha yako hususani maisha ya mwamini! ila leo ntaongelea jinisi gani dhambi imekua kikwazo cha uponyaji.....( SI UPONYAJI WA MWILI TU HATA WA KIROHO)
1 KIROHO
katika Yakobo 5:16 inasema "ungamaneni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa" jiulize swali kwamba kwa nini Mungu alisema muombeane ili mponywe ila kabla ya kuponywa, ameanza kwa kusema ungamaneni? Kama kuna kitu Mungu anachukia ulimwenguni basi ni dhambi. kuna sehemu kwenye biblia inasema "dhambi ni chukizo kwa Mungu" Mungu anachukia sana dhambi, ukisoma katika Mwanzo 6:5-6 inasema " Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila analowaza moyoni mwake baya tu siku zote. Bwana akaghairi kuwa amemfanya mwanadamu duniani akahuzunika moyo. yaani embu jaribu kufikiria hadi Mungu anajuta kwa nini alituumba! unaweza ukapata picha ni kwa kiasi gani anachukia maovu. sasa nilifundisha juu ya somo la kwanini unajidanganya mwenyewe? yaani unakuwa mnafiki mbele za Mungu, dhambi unaitaka, Mungu unampenda! vinaendana kwa karibu. unaposhilikilia dhambi ni ngumu kwako mpendwa kuponywa roho yako. inapofikia kipindi unaona uko vibaya kiroho na unahitaji uponyaji, kama bado hutaki kuacha maovu, tambua ya kwamba ni vigumu sana kupokea uponyaji wako.
Isaya 66:2b inasema" lakini mtu huyu ndiye ntakaye mwangalia mtu alie myonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu. Mungu anamwangalia mtu mnyenyekevu, dhami ufanyazo zinamzuia Mungu kutenda kitu katika maisha yako ya kiroho. mfano, mvuta bangi ameokoka anakuja kanisani kama kawaida tena vizuri ila akitoka anarudi vijiweni kwake anaendelea na bangi kama kawaida........mtu huyu hata ataombeje ili aache tatizo la kuvuta bangi itakua ngumu sana maana kwanza yeye mwenyewe bado anayoshauku ya kuendelea na hiyo dhambi hivyo ni ngumu kwa Roho mtakatifu kumsaidia maana hataki kusaidika ingawa anaomba.
2 Nyakati 7:14 inasema "ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe yao na kuiponya nchi yao......kwaiyo bado andiko hili linatudhihirishia kuwa dhambi ni kikwazo cha uponyaji. hapa Mungu anasema nitaiponya nchi ila kabla ya kuponya anataka tuache njia mbaya kwa maana ya toba.
2 KIMWILI
swala la pili hapa ni uponyaji wa kimwili yaani magonjwa yanayowasumbua watu. yupo mdada mmoja aliokoka mkutanoni kanisani kwetu ila alikua na mapepo yaliomsumbua mda mrefu sana kiasi cha kumpa magonjwa. tuliomba na kuomba paka! funa siku tulipokua tunaomba tuliwauliza yale mapepo kwanini hawataki kuondoka ndipo walitujibu kuwa ana vitu vyao na ndio maana hawataki kwenda.....tulipovichoma moto yule dada alifunguliwa palepale!
Mungu anapata kikwazo kukuponya maana umeishikilia dhambi nabado hutaki kuiacha. mapepo hawaoni sababu ya kukuacha wakati bado unajenga mazingira ya kukaa nao.
Zaburi 103:3 inasema " akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote" tunazidi kuona kuwa kabla ya kukuponya magonjwa yako kinachoanza ni kusamehewa kwanza. Mungu awezi kukusamehe na dhambi zako hata siku moja. ni either utubu na upate uponyaji au uendelee na dhambi na kuteseka katika magonjwa.
katika Mthayo 9:1-3 tunaona kuwa walipomleta yule mwenye kupooza akiwa kitandani, Yesu alisema "jipe moyo mkuu mwanangu, umesamehewa dhambi zako" Yesu alimsamehe dhambi zake kwamza aliharuhusu uponyaji maana kama nilivyosema hapo juu, dhambi ni kikwazo cha uponyaji. somaa popote pale hasa katika vitabu vya injili, Yesu alikua ana ponya na kumwambia huyo mtu kuwa asitende dhambi tena au anasamehe dhambi ili kuruhusu uponyaji ndani yake.
Kwaiyo mpendwa, dhambi ni kikwazo cha uponyaji wa kimwili na kiroho pia. dhambi imekua chanzo cha kutobarikiwa pia na kupata mafanikio katika maisha yetu.....
STAY INSPIRED!!!!!!!!

Saturday, January 9, 2016

SOMO: KWANINI UNAENDELEA KUJIDANGANYA MWENYEWE?


Katika ufunuo 3:15-16 anasema"nayajua matendo yako ya kuwa hu baridi wala hu moto, ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto basi kwa sababu una uvuguvugu wala hu baridi wala moto ntakutapika utoke katika kinywa changu.....
Wengi wetu tunaishi maisha ya uvuguvugu na ndiko kujidanganya
anaanza kwa kusema" NAYAJUA MATENDO YAKO" yaani Mungu anatujua kuliko tunavvyojijua na ndio maana hatumdanganyi yeye bali sisi wenyewe! unapojifanya umeokoka huku matendo yako hayaendani na mtu alieokoka, tambua unajidanganya wewe mwenyewe wala sio Mungu! kuna jamaa yangu niliienda kumshuudia, nilipenda jibu lake sana alisema amenielewa ila anaomba aendelee kujihakikisha kablbla ya kufanya maamuzi asije akawa anakuja kanisani kuniridhisha tu! kwa kweli nilifurahi sana si kwa ajili hataki kuokoka bali kwa ukweli na uwazi wake. ni heri ya huyo kuliko wewe unaeenda kanisani ili watu wakuone tu au kama desturi ya mkristo ila pombe kama kawaida, uzinzi kama kawaida, anasa kama kawaida na dhambi nyingi uzijuazo.
Kwanini nasema unajidanganya mwenyewe? mfano mtu anapo enda kuiba huwa anajua kuwa hakuna mtu anae mwona na ndio maana anavizia watu hawapo ndipo anaiba au mtu anapoenda guest, pengine anaenda sehemu ya mbali ili wanaomjua au wapendwa wenzake wasimwone lakini anasahau kuwa Mungu anamwona...na ndio maana kuna sehemu kwenye biblia anasema "YEYE AONAYE SIRINI" ina maana huwezi kumdanganya Mungu hata kidogo hata ufanyeje yeye bado anaona na anajua ya moyoni mwako.soma Isaya 29:15 "ole wao wanaojitahidi kumficha Bwana mashauri yao, na matendo yao yamo gizani nao husema, ni nani atuonaye? nani atujuaye?
Isaya 30:1 inasema" ole watoto waasi asema BWANA; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi" kwaiyo, pengine ulikua unafikiri kuwa Mungu hajui yale huyafanyayo sirini. nataka nikupe pole kwa kujidanganya mwenyewe muda wote huu. kwa kweli Mungu ana huruma sana hivi nilikuwa nawaza kama ndio ingekuwa zama za kina nuhu au sodoma na gomora sijui nani angepona? maana kipindi ile ilikuaa ni pale pale hakuwa na mjadala na mtu! leo tunashuudia wanakwaya wanaimba madhabahuni na huku bado ameshikiria mashauri yake, mpiga vyombo, tena anapiga chombo kwa ustadi mzuri sana ila anaendelea kutwanga dhambi kama kawaida...Mungu anatuvumilia akisubiri aone llabda kesho au kesho kutwa utatubu ila wapi!!!
Mathayo 15:7-9 inasema" enyi wanafiki ni vyema alivyo tabiri Isaya kwa habari zenu akisema watu hawa huniheshimu kwa midomo ila mioyo yao iko mbali nami nao wananiabudu bure wakifundisha maagizo yaliyo ya mwanadamu. je, ni mara ngapi umekua mnafiki mbele za Mungu? ni mara ngapi unamwabudu bure? mara ngapi unamuheshimu Mungu kwa mdomo tu? jibu unalo moyoni mwako!!!! sura ya 23:27 anasema" ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki! kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliopakwa chokaa nayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri bali ndani yamejaa mifupa ya wafu na uchafu wote" unaona Yesu alivyowafananisha waha mafarisayo wanafiki? na ndivyo wengi wetu leo tunaishi maisha ya unafiki tu!!!!
Yeremia 7:9-10 anasema " je! mtaiba na kuua na kuzini na kuapa kwa uongo na kumfukizia baali uvumba na kuifuta miungu mingine ambayo hamkuijua, kisha mtakuja na kusimama mbele zangu ktk nyumba hii iitwayo kwa jina langu na kusema tumepona ili mpate kufanya machukizo haya yote?
usiende kanisani kisa flani amesema au baba kakulazimisha, chukua hatua mwenyewe, badilika! baba atafurai kuwa unaenda kanisani, tena mchungaji atafarijika kwa kuwa unaongeza idadi ya waumini kanisani ila kumbuka wewe ndio utasimama kujibu mbele za Mungu wala sio baba au mama yako...kwa mfano mapepo mengine yanasababisha magonjwa sugu kwa mtu au unakuta mtu anavamiwa kila siku, kanisa mtaomba paka! ila sa nyingine ni jinsi mtu anavyojiweka, unapenda dhambi ni obvious na mapepo watakupenda kwasababu unawapenda!(sio wote)
Sitaki kumhukumu yeyote maana mimi sio Mkamilifu au Malaika kwamba sikosei la hasha! ila wote tunajijua maisha tunayoishi mbele za Mungu kama umechagua kuishi maisha ya unafiki, sawa! kama umechagua kumtumikia Mungu barikiwa sana! biblia inasema mwenye kufanya dhambi na afanye na mwenye kijitakasa na azidi kujitakasa......kama unaona dhambi ni nzuri kuliko Mungu, endelea kutumbua kwanza alafu ukiona sasa imetosha rudi anza upya kuliko kuendelea kuwa mnafiki! ni maombi yangu tufike mahali tumuogope Mungu......
STAY INSPIRED!!!!!!!!!!!

Tuesday, January 5, 2016

SOMO: TAMBUA VIZUIZI VYA MAENDELEO.


Bwana Yesu apewe sifa....leo ntaenda kufndisha juu ya somo la kutambua vizuizi vya maendeleo yako binafsi.
Kama Mkristo, upaswi kuwa maskini kabisa maana katika Mithali 8:18 anasema utajiri na heshima ziko kwangu, naam utajiri udunuo na haki. Zaburi 24:1 inchi na vyote viujazavyo ni mali ya Bwana. yako maandiko mengi yanayoonesha kuwa mtu wa Mungu hutakiwi kuwa maskini kabisa maana nijuavyo mimi Mungu ni Baba yetu na sisi kama watoto ni warithi wake.....sasa haiwezekani na kamwe haitotokea eti Baba ni tajiri alafu mtoto ni maskini........uliona wap? Mfano ikitokea baba yako amekua milionea, pengine hata kusoma unaweza ukaacha maana unajua hata iweje huwezi kulala njaa, kukosa maitaji n.k.
sasa zipo sababu kwanini watu wa Mungu hatufanikiwi. kama somo linavyo someka hapo juu, kuna vitu vinazuia maendeleo yako Mtu wa Mungu....sa nyingine sio kwamba umevamiwa na pepo hapana! sikatai kuna maroho ya umaskini na ufukara yanayofuatilia watu wa Mungu ila kuna vitu ni vya kuchukua hatua tu na mafanikio yatakuja. haleluyah!
1.KUTOKUA NA MALENGO(nia)
Ni wachache sana wanaofanya vitu kwa kuweka nia na malengo juu ya hivyo vitu. wapo watu anasoma lakini hajui hata anasoma ili iweje au anataka kuwa nani hapo badae. watu we dont have FOCUS on the things ahead. leo tunashuudia watu ndoa zinawashinda kwa sababu wanashindwa kumudu gharama za maisha, ni kwasababu hapo awali walikua wakiishi tu bila kujali mbele yake itakuaje mwishowe wanakurupuka kwa sababu kila mtu anaoa basi naye anatimiza wajibu.....mfano mzuri ni katika mpira, wanaopenda watakubaliana na mimi...unajua kwa nini nchi za wenzetu ziko juu na zinafanikiwa? ni malengo na nia waliojiwekea toka awali. waliandaa vijana ambao sasa hivi ndo wanatisha..angalia Tanzania, sio kwamba tuna pepo la hasha! hatuna mipango ya badae kila kukicha wanataka Timu iamke asubuhi moja tu alfu ghafla wajikute wako kombe la dunia.(jiulize kuwa kina samatta na ulimwengu kwanini wanafanikiwa)
kutokua na malengo ni kama mtu anaejenga nyumba bila kuwa na ramani...sijawai kuona na sijui hiyo nyumba itakuaje! Luka 14:28 inasema maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya kumalizia?. Yesu alitoa mfano huu ukiwa ni dhairi kuwa unatakiwa kuwa na lengo au nia ya kufanya kitu.
2.UVIVU/KUPENDA USINGIZI
unakuta tu mtu mvivu anapenda kulala balaa alafu huyohuyo mtu analalamika hana mafanikio anaomba maombi. nakwambia tutamuombea hadi nywele zitanyonyoka! Mithali 6:9-10 ewe mvivu utalala hata lini?utaondoka lini katika usingizi wako? sura ya 13:4 nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu. 10:4 atendaye mambo kwa mkono wa mlegevu huwa maskini. bali mkono wake aliye na bidii hujitajirisha. 20:13 usipende usingizi usije ukawa maskini fumbua macho yako nawe utashiba chakula.
Biblia imesema sana juu ya watu wavivu, kupenda usingizi. kwaiyo mwenye bidii lazima afanikiwe.siku tafuta muda wako nenda kwa matajiri unao wajua watakwambia, lazima walikua na bidii. ndio kuna watu wanatajirika kwa urithi ila bado kuna bidii atafanya kumantain utajiri ule awezi kukaa tu. sasa niambie hapo kama unaitaji maombi wakati we ni mvivu na unapenda usingizi? kama we si mvivu na umefanya kila liwezekanalo alafu hali ni ileile, hapo sasa maombi yanaitajika.
MAWAZO HASI(NEGATIVE THOUGHTS)
ninaposema negative thoughts yaani mtu badala ya kuwaza mambo ya kimaendeleo, anawaza kumsema mtu, kulipiza kisasi,anawaza anasa tu, na vitu vingine vingi.Mithali 21:5 mawazo ya mwenye bidii huelekea utajiri tu, bali kila mwenye pupa huelekea huitaji. hili linaendana na hapo juu, mtu mvivu awezi waza maendeleo ye ni kuwaza ale kwa mpendwa gani kwa siku hiyo, hawezi waza kufanya kazi. 28:19 alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele bali afuataye mambo ya upuuzi atapata umaskini wa kumtosha. napapenda hapa maana amesema vizuri sana. yaani afuataye mabo ya upuuzi ina maana upuuzi anao uwaza kama nilivyosema hapo juu.kwaiyo like uwazacho kina impact kubwa sana katika maisha yako ukiwaza upuuzi basi ndivyo utakavyo kuwa ukiwaza maendeleo utayapata maana ndicho uwazacho mfano mtu anawaza kufelifeli tu katika masomo yake ni lazima atakua wa kufeli maana akishawaza moyoni mwake na mentality yake sasa inakua hivyo hivyo na mwisho wa siku hata kusoma inakua shida.......
3.KUTOKUA NA (STS)
STS ni
-SELF DISCIPLINE(nidhamu binafsi)
-TIMEMAHAGEMENT(kukomboa wakati)
-SAVING(kujiwekea akiba)
niliona kuwa vitu hivi vina humimu mkubwa sana katika kuleta maendeleo yako binafsi. wengi wetu leo hatuna nidhamu binafsi, hatukomboi wakati, na hatujiwekei akiba.
TIME MANAGEMENT(kukomboa wakati)
waefeso 5:15-16 basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu waio na hekima bali kama watu wenye hekima. mkiukomboa wakati kwa maana zama hizi ni za uovu. Kol 4:5 enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.
kwaiyo wakati ni jambo moja la msingi sana. kuna msemo sa hivi mtu anasema eti naenda beach kupetezapoteza muda! aisee kama ulikua unasema hivyo acha kabisa, time is not to be wasted!
unapopangilia mda wako unaokoa vingi sana.......Watanzania swala la mda linatugalimu coz tumeka waswahili sana hatutunzi muda. we angalia kwa mfano we mwenywe shuleni ukipangilia time table yako binafsi ya kujisomea kuifuata ni shida.
SELF DISPLINE(nidhamu binafsi)
nidhamu binafsi ni kuwa na utaratibu mzuri wa kuendesha maisha yako. kuna msemo unasema usipo jiheshimu uwezi kuheshimiwa.
2 Thes 3:11 maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu hawana shuguli zao wenyewe lakini wanajishugulisha na mambo ya wengine. kwaiyo how do you expect a person like that awe na maendeleo? mtu hana utaratibu wa kujiendesha hajui afanye nini ni ngumu kufanikiwa.
SAVING( akiba)
ni wangapi leo tuna tabia ya kujiwekea akiba? neno la Mungu linasema Mithali 6:8 lakini hujiwekea akiba ya chakula watati wa jua hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. ukijizoeza kuweka akiba sasa hivi uwezi kupata tatizo hapo badae maana vipo vya kutosha. sa hv unakuta watu wanaishiwa kupita maelezo na ndio maana kukopana kumezidi. mi mwenyewe ni lisumbuka sana na hili tatizo paka pale nilipogundua. akiba ni jambo muhimu sana wapendwa!
STAY INSPIRED!!!!!!!!!

Sunday, January 3, 2016

SOMO: JIFUNZE KUACHILIA ILI MUNGU AKUSAMEHE.


Watu wengi atujui maana ya kusamehe na kuachilia. katika kichwa cha habari hapo juu nimetumia neno kuachilia, maana unaweza ukasamehe na usiachilie.inawezekana ushawai kusikia ule msemo kwamba nimekusamehe ila sito kusahau. Mungu anataka tuachilie sio kusamehe peke yake. kuachilia ni kusamehe na kutokumbuka kamwe.
Hivi pata picha kama Mungu asinge kusamehe wewe ungekua wapi? sasa swali linakuja unashindwaje kusamsamehe mwenzako?? Mungu ni zaidi ya mzazi kwetu,kuna wengi leo wamefukuza na wazazi wao au pengine wamekorofishana na hawapatani hadi leo sababu labda kuna kosa mmoja wao alimfanyia mwenzake. ila kwa Mungu hali ni tofauti, unazidi kumuudhi kila kukicha lakini yeye ana kusamehe tu. jana ulikua unaiba na leo uko kanisani, yeye anasamehe, unajifanya umeokoka ila una mambo yako ya chinichini, yeye anasamehe tu.
swali langu ni kama Mungu anakusamehe na kusahau yale uliofanya jana, mbona tunashindwa kuwasamehe waliotukosea?
Wengi tunaijua sala ya Baba yetu na pengine tumeiimba sana tukiwa sunday school ya watoto na pengine hata leo tunazidi kuziimba. ukisoma Math 6:9 anasema Baba yetu ulie mbinguni jina lako litukuzwe.............................................................................................sasa, ukiendelea mstari wa 12 unasema utusamehe deni zetu kama na sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu!!! hebu jaribu kutafakari,nikweli unachosema? au kwasababu ni sala na imeandikwa katika Biblia basi unasema tu? Maana yake hapo unamwambia Mungu akusamehe wewe kwasababu juzi na wewe uliwasamehe waliokukosea. sasa swali linakuja Mbona wewe hukusamehe sasa kwanini unataka wewe usamehewe? Ni ngumu watumishi si kama tunavyodhani....Luka 17:3-4 anasema jilindeni ndugu yako akikosa mwonye, akitubu msamehe. na kama akikukosa mara saba ktk siku moja na kurudi kwako mara saba akisema nimetubu, msamehe. sikia hapo juu Yesu alisema hata akikukosa mara saba, Petro aliambiwa samehe saba mara sabini, of coz hakuna mtu akosae kiasi hicho kwa siku lakini Yesu alikua anajaribu kuonesha kuwa no matter makosa yanayofanywa na watu kila siku kwako, wewe samehe tu. kwaiyo yesu alivyosema saba mara sabini that means ni 470.....sasa nani anaweza kufanya hivyo ingawa kosa moja tu ulilofanyiwa mwaka jana na ndugu yako umelishikilia moyoni mwako hutaki hata kumwona!!!!
Marko 11:25 nanyi kila msimamapo na kusali, sameheni mkiwa neno juu ya mtu, ili Baba yenu alie mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.26 lakini kama ninyi hamsamehe wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. nimependa aliposema kuwa sameheni ili na Baba awasamehe na ninyi makosa yenu. kwaiyo unaweza kuona kuwa unaposamehe Mungu nae anakusame makosa yako. sa nyingine tumekuwa hatujibiwi maombi yetu maana tunamwendea Mungu wakati mioyo yetu imebeba machungu na machukio juu ya watu, hapo juu amesema msimamapo na kusali. kwaiyo kumbe kutokusamehe inaweza ikawa chanzo cha kutojibiwa maombi. unaweza ukamkuta mtu anavyotubu mbele za Mungu analia na kuomboleza huku akimbembeleza Mungu amsamehe, neno liko wazi samehe usamehewe basi yaani fomula ya Mungu ni ndogo sana.
Math 5:7 heri wenye rehema maana hao watapata rehema.
kuna wapendwa wansema wameokoka na mbinguni wanaenda ila ukiwakuta hata kanisani hawaongei ni chuki kwa kwenda mbele...sasa sijui ni mbingu ipi hiyo ya watu wa namna hiyo. kwanza ni jambo la ajabu hivi inakuaje unachuki na mpendwa mwenzako? na mataifa watafanyaje? Kanisa la leo upendo hakuna, Umoja hakuna...watu wanahama makanisa eti kisa mpendwa mwenzake kamkwaza! mambo mengine sio ya kukemea, unakuta mtu anaomba Mungu amsaidie asiwe na hasira alafu kesho na keshokutwa mtu akikukwaza una kasirika. badae unaenda kwa mchungaji akuombee, uwezi pona. hilo swala ni lakucontrol wala si kuomba. chukua hatua ujicontrol alafu katika kujicontrol kwako ndipo umuombe Mungu akusaidie.
4give everything that happened last year and the past years....this year is going to be a prosperous year for you,only if you 4give and start a new page in your life!!!!
STAY INSPIRED..!!!!!

Saturday, January 2, 2016

SOMO: WEWE NI WA THAMANI MBELE ZA MUNGU.


Bwana asifiwe, ni furaha ilioje kuuona mwaka. Tunamshukuru Mungu kwa kweli maana ni wengi walitamani. kwa mwaka huu wa 2016, nimeona niendelee na mtiririko wangu wa masomo na leo ntaenda kufundisha juu ya uthamani wako kama mkristo hasa kijana ulieokoka.
UTANGULIZI
Mtu ukishaokoka lazima utambue kuwa wewe ni wa thamani mbele za Mungu. Mungu anatuona kama wa thamani sana mbele zake na ndio maana alisema atakae kugusa anagusa mboni yake! kwaiyo unaweza pata picha juu ya thamani ulionayo mbele za Mungu. 
USIHARIBU UJANA WAKO.
Vijana wengi tunapoteza thamani yetu mbele za Mungu kwa kuharibu ujana wetu.
1. ZINAA, hivi ushawai kukaa na kufikiri kwamba unaharibu usichana au uwanaume wako? kwa mfano mtu ukiwa na mchumba ukazini ane akakuacha, akaja mwingine ukazini nae, mwingine na mwingine...pata picha kama utakua na utofauti na anae ujiuza kama ni tofauti ni kwamba yeye hana watu maalumu ila wewe unao basi hiyo ndio tofauti. 1Thes 4:4 inasema kila mmoja wenu na ajue kuuweka mwili wake katika utakatifu. 1Kor 6:18 inasema ikimbieni zinaakila dhambi aitendayo mwanadamuni ne ya mwili wake ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake, ukiendelea mstari 20 inasema maana mlinunuliwa kwa thamani. sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu. so kitu kikubwa hapa ni zinaa. vijana wengi leo wanashindwa kujizuia na shetani kwakua anajua huu ni udhaifu wa vijana kwa kweli anakesha usiku na mchana akihakikisha anadhoofisha vijana. nilikutana na mtu akasema kwamba kwa kweli yeye asipo zini kuna kitu kinapungua ndani yake na anahisi atakufa. nataka nikuhakikishie kwamba zinaa inazuilika na wala hautakufa, zinaa sio chakula kwamba usipokula utakufa au utadhoofika LA HASHA! sio kwamba nasema haya tu, mimi mwenyewe nilidhani hivyo ila baada ya kukombolewa hakika naanza kujuta kwa nini nilikua nazini kabla ya wakati wa ndoa.
nakumbuka kuna rafiki yangu aliniambia kua ukizini jua kua unaharibu maisha ya mke wa mtu ajae.....mithali 6:32 inasema mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa, afanya jambo linalomwangamiza nafsi yake. wimbo ulio bora 3:5 enyi binti za yerusalemu msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha hata yatakapoona vyema yenyewe.
KWANINI ZINAA?
I)TAMAA ZA MWILINI, Mithali 6:25 inasema usitamani uzuri wake moyoni mwako usikubali akunase kwa kope za macho yake.1Tim 2:22 inasema zikimbieni tamaa za ujanani ukafuate haki. 1Petro 2:11 inasema wapenzi nawasihi kama wapitai ziepukeni tamaa za mwilini zipinganazo na roho. Kwaiyo hapa tunaona chanzo kubwa la kuanguka katika dhambi ya zinaa ni tamaa ya mwilini....unaweza ukasema mbona nashindwa kuicontrol? angalia Rum 8:13. sababu ni kuishi katika mwili, laiti kama tukiyafisha mambo ya mwili kwa Roho Mtakatifu hakika utaweza.
ii) MAMBO YA DUNIA, usitegemee kuwa utashinda majaribu ukiwa bado unaipenda dunia..1Yoh 2:15 msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia. mithali kama nilivyosema uwezi ukashinda majaribu wakati unayapenda, unakuta kijana ameokoka vizuri tu lakini hana tofauti na ambao bado hawajaokoka kwanini? ni kwa sababu yale alioyashikilia bado, yanaendelea kumzonga zonga mfano umeokoka lakini bado disko unataka kwenda, bar unaendelea ila kwa kisingizio unakunywa soda tu, bado manyimbo ya dunia unayo tena kwenye simu yako...labda nikufumbue., nyimbo hizo hazina utukufu na kila kinachoimbwa katika nyimbo hizo kuna maroho kama nyimbo ni mapenzi basi roho ya mapenzi haiwezi ikakuacha ng'o!
iii) marafiki/mahusiano, wengi wamepotea hasa kwenye sehemu hii. 1:10 mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi wewe usikubali. 2Wak 6:14 msifungwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi ilivyo sawasawa kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? tena panashirika gani kati ya nuru na giza? mithali 24:1 usiwahusudu watu waovu wala usitamani kuwa pamoja nao. kwaiyo marafiki wana ushawishi mkubwa sana kwako kama ulikua hujui. yaani kama rafiki yako hataki kuacha dhambi kwa vyovyote ukishirikiana nae lazima nawwe utashawishika tu. mithali 13:30 inasema enenda pamoja na wenye hekima uatakuwa na hekima. hivyo hivyo ukienenda na wafanyao dhambi nawe utakua mtenda dhambi. ukisoma Mwanzo 34:1 utaona jinsi dina alivyo shawishika na marafiki zake atakuvunja usichana wake maana alikua hamjui mwanaume.
AINA ZA UPENDO
nataka kuongelea aina za upendo maana viana wengi tunakosea sana tukidhani tunapendwa kumbe sio.
1.UPENDO WA TAMAA, upendo huu ndo umekua sababu kubwa sana ya watu kuumia na kuumizwa katika mahusiano.....hapo juu nimeongelea tamaa, upendo wa tamaa unaanzia machoni na si moyoni n baada ya macho kuona unawasiliana na mwili wako ndipo unapohisi kuwa umependa kumbe umetamani. mfano mkaka anaweza kumwona mdada barabarani akamfata na kumwambia kuwa na kupenda...hapo dada unatakiwa kujua hiyo ni tamaa upendo wa kweli si wa ghafla.....1Samweli 13:1 tunaona jinsi amnoni alivyompenda dada yake tamari. ule haukua upendo wa kweli ulikua ni tamaa na ndio maana ukisoma mstari wa 15 amnoni akamchukia machukio makuu sana. mkaka akishakupenda, ukikubali akishazini na wewe kama ilikua tamaa lazima atakuacha tu maana hicho ndicho kilicho msukuma kwako. na ndio maana nawashauri wa dada ukiona uko na mtu na anakulazimisha mzini kataa tena mkimbie, maana upendo wa kweli huvumilia.
2.UPENDO WA HISIA, Unaweza ukashangaa lakini kuna upendo wa hisia. huu unakuja pale unapomwona mtu na kudhani unampenda ila huna uwakika. yaani unakua unahisi unampenda ila uwakika huna...sasa ushauri wangu hapa ni kwamba ukihisi kua unampenda mtu usikurupuke paka pale utakapokua na uwakika maana inawezekana ikawa no mwanzo wa kuharibu future yako. mfano kama ni mdada ukahhisi unampenda mkaka na ukamwambia inawezekana huyo kaka yeye akupendi na mwisho wa siku mabo ni yaleyale ya amnoni na tamari........atakuchezea na kukuacha.
3.UPENDO WA KWELI,huu unaanzia moyoni ukiangalia 1Petro 3:4 anasema na kuwe na utu moyoni usioonekana, ktk mapambo yasiyo haribika yaani roho ya upole na utulivu iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 1kor 13:1-13 yaani mimi naupenda sana maana characheristics za true love ziko hapa. mstari wa 4upendo huvumilia, hufadhili, hautakabari, haujivuni, haukosi kuwa na adabu, haufuati mambo yake. unajua ni tatizo letu tu sisi vijana lakini unaweza ukaomba na Mungu akakupa mtu sahihi wa maisha yako sasa tatizo linakuja tunaomba wakati tupo kwene mahusiano tayari.