Saturday, January 9, 2016

SOMO: KWANINI UNAENDELEA KUJIDANGANYA MWENYEWE?


Katika ufunuo 3:15-16 anasema"nayajua matendo yako ya kuwa hu baridi wala hu moto, ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto basi kwa sababu una uvuguvugu wala hu baridi wala moto ntakutapika utoke katika kinywa changu.....
Wengi wetu tunaishi maisha ya uvuguvugu na ndiko kujidanganya
anaanza kwa kusema" NAYAJUA MATENDO YAKO" yaani Mungu anatujua kuliko tunavvyojijua na ndio maana hatumdanganyi yeye bali sisi wenyewe! unapojifanya umeokoka huku matendo yako hayaendani na mtu alieokoka, tambua unajidanganya wewe mwenyewe wala sio Mungu! kuna jamaa yangu niliienda kumshuudia, nilipenda jibu lake sana alisema amenielewa ila anaomba aendelee kujihakikisha kablbla ya kufanya maamuzi asije akawa anakuja kanisani kuniridhisha tu! kwa kweli nilifurahi sana si kwa ajili hataki kuokoka bali kwa ukweli na uwazi wake. ni heri ya huyo kuliko wewe unaeenda kanisani ili watu wakuone tu au kama desturi ya mkristo ila pombe kama kawaida, uzinzi kama kawaida, anasa kama kawaida na dhambi nyingi uzijuazo.
Kwanini nasema unajidanganya mwenyewe? mfano mtu anapo enda kuiba huwa anajua kuwa hakuna mtu anae mwona na ndio maana anavizia watu hawapo ndipo anaiba au mtu anapoenda guest, pengine anaenda sehemu ya mbali ili wanaomjua au wapendwa wenzake wasimwone lakini anasahau kuwa Mungu anamwona...na ndio maana kuna sehemu kwenye biblia anasema "YEYE AONAYE SIRINI" ina maana huwezi kumdanganya Mungu hata kidogo hata ufanyeje yeye bado anaona na anajua ya moyoni mwako.soma Isaya 29:15 "ole wao wanaojitahidi kumficha Bwana mashauri yao, na matendo yao yamo gizani nao husema, ni nani atuonaye? nani atujuaye?
Isaya 30:1 inasema" ole watoto waasi asema BWANA; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi" kwaiyo, pengine ulikua unafikiri kuwa Mungu hajui yale huyafanyayo sirini. nataka nikupe pole kwa kujidanganya mwenyewe muda wote huu. kwa kweli Mungu ana huruma sana hivi nilikuwa nawaza kama ndio ingekuwa zama za kina nuhu au sodoma na gomora sijui nani angepona? maana kipindi ile ilikuaa ni pale pale hakuwa na mjadala na mtu! leo tunashuudia wanakwaya wanaimba madhabahuni na huku bado ameshikiria mashauri yake, mpiga vyombo, tena anapiga chombo kwa ustadi mzuri sana ila anaendelea kutwanga dhambi kama kawaida...Mungu anatuvumilia akisubiri aone llabda kesho au kesho kutwa utatubu ila wapi!!!
Mathayo 15:7-9 inasema" enyi wanafiki ni vyema alivyo tabiri Isaya kwa habari zenu akisema watu hawa huniheshimu kwa midomo ila mioyo yao iko mbali nami nao wananiabudu bure wakifundisha maagizo yaliyo ya mwanadamu. je, ni mara ngapi umekua mnafiki mbele za Mungu? ni mara ngapi unamwabudu bure? mara ngapi unamuheshimu Mungu kwa mdomo tu? jibu unalo moyoni mwako!!!! sura ya 23:27 anasema" ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki! kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliopakwa chokaa nayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri bali ndani yamejaa mifupa ya wafu na uchafu wote" unaona Yesu alivyowafananisha waha mafarisayo wanafiki? na ndivyo wengi wetu leo tunaishi maisha ya unafiki tu!!!!
Yeremia 7:9-10 anasema " je! mtaiba na kuua na kuzini na kuapa kwa uongo na kumfukizia baali uvumba na kuifuta miungu mingine ambayo hamkuijua, kisha mtakuja na kusimama mbele zangu ktk nyumba hii iitwayo kwa jina langu na kusema tumepona ili mpate kufanya machukizo haya yote?
usiende kanisani kisa flani amesema au baba kakulazimisha, chukua hatua mwenyewe, badilika! baba atafurai kuwa unaenda kanisani, tena mchungaji atafarijika kwa kuwa unaongeza idadi ya waumini kanisani ila kumbuka wewe ndio utasimama kujibu mbele za Mungu wala sio baba au mama yako...kwa mfano mapepo mengine yanasababisha magonjwa sugu kwa mtu au unakuta mtu anavamiwa kila siku, kanisa mtaomba paka! ila sa nyingine ni jinsi mtu anavyojiweka, unapenda dhambi ni obvious na mapepo watakupenda kwasababu unawapenda!(sio wote)
Sitaki kumhukumu yeyote maana mimi sio Mkamilifu au Malaika kwamba sikosei la hasha! ila wote tunajijua maisha tunayoishi mbele za Mungu kama umechagua kuishi maisha ya unafiki, sawa! kama umechagua kumtumikia Mungu barikiwa sana! biblia inasema mwenye kufanya dhambi na afanye na mwenye kijitakasa na azidi kujitakasa......kama unaona dhambi ni nzuri kuliko Mungu, endelea kutumbua kwanza alafu ukiona sasa imetosha rudi anza upya kuliko kuendelea kuwa mnafiki! ni maombi yangu tufike mahali tumuogope Mungu......
STAY INSPIRED!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment