Sunday, January 31, 2016

SOMO: JIFUNZE KUMUHESHIMU MUNGU KWA MATENDO YAKO.


Shalom watu wa Mungu!
Ni jambo la kawaida kabisa mdogo kumheshimu mkubwa, kama wewe na mimi tunavyo waheshimu wazazi wetu na kama neno lisemavyo "waheshimu baba na mama yako upate kuishi siku nyingi duniani"
Leo ntaongelea tatizo ambalo sisi kama watoto tunalisahau au pengine tumelisahau maishani mwetu na tunaona kila kitu ni sawa tu. Wengi tunajisahau sana na setani amekuwa akitujanjia sana kupitia sehemu hiyo.
Kama somo langu linavyosema, ni kweli tunamheshimu Mungu sana tu ila tatizo linakuja, je hiyo heshima tunayompa ni kwa matendo yetu au ni maneno tu?????
Mathayo 15:8 inasema" watu hawa huniheshimu kwa midomo ila mioyo yao iko mbali nami, nao wananiabudu bure wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya mwanadamu. tunaona hapa inavyosema, kumbe kuna watu wanaomheshimu Mungu kwa midomo tu! ni sawa na unavyo waamkiaga wakubwa zako au wazazi wako ila ukitumwa huendi, ukiambiwa usifanye hiki unafanya lakini asubui ikifika, shikamoo iko palepale................
Isaya 29:13 inasema" Bwana akanena kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao ila mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walichonacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa. kuna siku nilifundisha juu ya kumpendeza Mungu na si mwanadamu. ukiangalia kwa makini katika mstari huu anamalizia anasema "na kicho chao ni maagizo ya mwanadamu" yaani kuna watu wanaonekana wanamheshimu Mungu kwa sababu wanaogopa kusemwa na pengine wachungaji wao au wazazi.
Mithali 3:9 inaema" mheshimu bwana kwa mali yako na kwa malimbuko ya mazao yako yote" mbaya zaidi wachungaji wanapoongelea swala hili, watu tumekuwa tukiona kama vile wako wanajipigia debe ili wapate fedha, LA HASHA! ndugu kwa kufanya hivi ni kumheshimu Mungu kwa matendo. kwanza ni chanzo cha Baraka, endelea kusoma mstari wa 10, alafu utasoma Malaki 3:10 uone kama huwa tunapiga stori. kumbuka anania na safira, walikufa palepale baada ya kuiba sehemu ya kumi ambayo walitakiwa kutoa(ukitoa nusu, usipotoa kabisa, Mungu anakuona mwizi tu)....Mungu ana huruma sana fikiria kama ingekuwa enzi za kina safira wangekufa wangapi leo hii???
sifundishi kutoa zaka ila nasema kwa sababu huko ndiko kumheshimu Mungu kwa matendo!
sifundishi kutoa zaka ila nasema kwa sababu huko ndiko kumheshimu Mungu kwa matendo.
tumalizie kwa kusoma Ezekiel 33:31 inasema" nao huja kwako kama watu wajavyo nao hukaa mbele yako kama watu wangu nao husikia maneno yako wasiyatende maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi. lakini mioyo yao inatafuta faida yao. unaona anavyozidi kusema hapa.....maana yake halisi ni unafiki! maana watu hawa hujifanya kama wanamheshimu Mungu kumbe hakuna kitu ndani yao. ni maombi yangu kuwa, kama ulikua unamheshimu Mungu kwa mdomo tu ni wakati wa kugeuka na kufanaya kwa matendo,
Kumbuka kutomheshimu Mungu kwa matendo, "ni sawa na unavyo waamkiaga wakubwa zako au wazazi wako ila ukitumwa huendi, ukiambiwa usifanye hiki unafanya lakini asubui ikifika, shikamoo iko palepale................
STAY INSPIRED!!!!!!!

No comments:

Post a Comment