Sunday, January 17, 2016

SOMO:USIPO BOMOA MSINGI WA DHAMBI ULIOUJENGENGA, UTAENDELEA KUKUTAFUNA.


Kama umeshaokoka na unaendelea kutenda yale uliokua unatenda tambua ya kwamba unaendelea kushindilia msingi wa dhambi badala ya kubomoa na ndio maana ni rahisi kuvamiwa.
2Petro 2:20 inasema "kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na mwokozi Yesu kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Hapa tunaambiwa kuwa wale waliokimbia machafu ya dunia kwa maana ya kwamba mimi na wewe tuliogeuka tukaacha dhambi na kuokoka anasema kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho hua mbaya zaidi........
kichwa cha somo langu ni usipo bomoa msingi wa dhambi ulioujenga, utaendelea kukutafuna! ni kweli tunapoachana na mambo ya dunia tutambue kuwa shetani hafurahii kabisa na ndio maana mtu anapookoka kuna kuwa na upinzani wa mambo ya kiroho zaidi maana shetani yuko kuhakikisha kuwa unashindwa tu. sasa tulipokua upande wa ulimwengu yaani shetani kuna dhambi ambazo tulizoelea kuzifanya mfano mtu alikua mlevi wa pombe tena wakupindukia, sasa anapookoka na kuachana na ulevi, lile pepo la ulevi likimtoka haliendi mbali bado linaendelea kumnyemelea na ndio maana ni rahisi kwa wachanga kiroho yaani waliokoka karibuni kurudi kule walipotoka, kwanini? kwa sababu mapepo bado wananyemelea kilicho kuwa chao..
Nakumbuka kuna dada fulani alifundisha kuhusu kuvunja maagano na laana uliyoweka na shetani...unaweza ukashangaa ni maagano gani ulioweka mfano ulipokua hujaokoka kutoa mimba ilikua kawaida, unapookoka na kuolewa unaweza ukashangaa unakua tasa(sio kwamba mtu akiwa tasa hii ndo sababu hapana) sasa huo utasa unaweza ukasababishwa na wale mapepo maana ulipokuwa kwao ulikua unatoa mimba sasa baada ya kubadilika wanaamua kukufunga tumbo lako!
Luka 11:24-26 inasema " pepo mchafu amtokapo mtu hupitia mahali pasipo maji akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona husema nitarudi nyumba yangu niliyotoka, hata afikapo akiona imefagiliwa na kupambwa ndipo huenda akachukua pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe wakaingia na kukaa humo na mtu huyo hali yake ya kwanza huwa mbaya kuliko ya kwanza. nadhani unaweza ukapata mwanga juu ya kile ninachoongea. kwaiyo pepo anapomtoka mtu, huwa haendi mbali anaendelea kunyemelea kilicho kuwa chake na ndipo maandiko tuliyosoma yanasema akikuta imefagiliwa na kupambwa huenda akachukua wengine saba tena wabaya kuliko yeye alafu anamalizia anasema hali yake ya kwanza huwa mbaya zaidi kuliko ya kwanza..........kwaiyo mpendwa wewe unaweza ukaona ni kawaida tu na pengine ukashangaa kwanini mtu anaanguka katika dhambi tena kirahisi sana, ni kwa sababu hajabomoa msingi wa dhambi alioujenga na kujiwekea ulinzi wa kutosha.
katika Yohana 5:14 inasema "baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu akamwambia, angalia umekuwa mzima usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi.....kwaiyo Yesu alijua kwamba kama mtu yule ataendelea kutenda dhambi ni dhahiri wale mapepo watarudi tu.
Joshua 7:12 Mungu alimwambia joshua kuwa hatakuwa pamoja na wana waisrael kama wasipokiharibu kile walichokuwa nacho kilichoweka wakfu. Ukisoma sura yote ya 7 utagundua kuwa ile dhambi ya wizi iliyofanywa na wana israel kwa kuiba vvile vitu ndo ilikua inaendelea kuwatafuna na ndio maana walikua wakipigwa kila wanapoenda vitani. mstari wa 11 Mungu anawmambia Joshua kuwa asisumbuke kulia kwa sababu israeli wametenda dhambi. ila ukiendelea utaona kuwa baada ya kuharibu kile walichokiiba Mungu alikua pamoja nao na waliendelea kushinda vitani.
kwaiyo tusipobomoa yale tuliyoyaacha na kuendelea kuyatenda yataendelea kututafuna.
STAY INSPIRED!!!!!!!

No comments:

Post a Comment