Sunday, November 29, 2015

SOMO:TUNAMZUIA MUNGU KUTUBARIKI KWA SABABU YA MAOVU YETU.

       Bwana yesu apewe sifa wapenzi wasomaji.........napenda kumshukuru Mungu kwa nafasi alionipa tena, Katika mwendelezo wa masomo yangu, leo nitafundisha juu ya ni kwanini watu wa Mungu wengi hawabarikiwi.
     Kwanza lazima tujue kuwa baraka ni haki yako kabisa kwa sababu ni ahadi ya Mungu mwenyewe, ukisoma kumb 28 utaona jinsi gani ahadi hizo zimetolewa. Sasa mtu unaweza ukajiuliza inakuaje nasema ni haki ya mwamini wakati wewe umekua ni Mtu wa kuwapigia makofi wenzio kanisani wakati  wanashuudia baraka walizopata either Mungu kawasaidia kununua gari, kupata kazi, kujenga nyumba, n.k
        Jibu ni rahisi sana....binafsi namshukuru Mungu kwa sababu amenifunulia siri hii na imekua msaada mkubwa sana katika maisha yangu.
         Wapendwa sisi wenyewe ni chanzo cha kuzuia baraka hizi..........iko hivi, kama kuna kitu ambacho Mungu anapenda kutoka kwetu, basi ni utii wetu kwake(anapenda kuabudiwa, kuheshimiwa). Sasa tatito linaanzia hapa Mtu anataka Mungu ambariki wakati yeye hataki kumtii au kumheshimu. tusome Isaya 59:1-2''tazama mkono wa bwana haukupunguka hata usiweze kukuokoa wala sikio lake sio zito lisiweze kusikia, lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na Mungu na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Jamani haya maandiko nayapenda kwasababu yako wazi sana. yaani ukianzia mstari wa pili anasema, lakini maovu yenu na dhambi zenu zimeuficha uso wake na zimewafarakanisha. kwaiyo tunaona kabisa Mungu ashindwi kukubariki ila dhambi zako ni chukizo mbele zake na ndio kwazo la yeye kukubariki.
     Tusome tene Isaya 1:19'' kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi'' bado anasisitiza kitu   kimoja (UTII). kama nilivyosema hapo juu Mungu ndio kitu anapenda yaani ukimuheshimu ni lazima baraka zitakuja tu.
      Saa nyingine sio lazima hata kuomba, naomba unielewe sisemi kwamba usiombe hapana maombi ni muhimu sana na ndio silaha yetu ila ukijishugulisha na Mungu , yeye anajishugulisha na wewe kwa mfano Mtoto akiwa watii kwa wazazi kiasi cha kumfurahisha, utakuta siku mzazi anampa Mtoto labda zawadi au hela ya matumizi bila hata ya Mtoto yule kuomba. mimi imewahi kunitokea naamini na baadhi yetu pia. 2Nyakati 7:14'' ikiwa Watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi zao na kuiponya nchi''. Haya hapa tuna vitu vitatu, moja ni kijinyenyekesha na kuomba, mbili ni kutafuta uso wa Mungu, tatu ni kuacha njia mbaya. yeye(Mungu) sasa atachofanya, atasikia, atasamehe dhambi na kuponya. Kwaiyo unaitaji nini zaidi maana hapa mstari uko wazi kabisa wajibu wako na wajibu wa Mungu kwako.
      Zaburi 1:1-3 ukiangalia inasema ana heri mtu yule asiekwenda katika shauri la wasio haki, ukisoma biblia ya kiingereza inasema '' BLESSED IS THE MAN'' kwaiyo mtu asieenda katika dhambi amebarikiwa. mstari wa tatu unasema na kila alitendalo litafanikiwa............
     Wapendwa mimi mwenyewe ni shuhuda wa mambo ninayo yasema wala sisemi tu kwa sababu Mungu amenipa somo hili, la hasha! baada ya kupewa somo hili nilijirekebisha pale nilipokosea na  kwa kweli namuona Mungu sana katika Maisha yangu , kuna mambo najikuta yanatokea hadi nashangaa kwasababu hata mengine sikuomba ila nabaki kumshukuru.
    Ndugu mpendwa nawasihi katika Bwana , ifike muda tuache sasa kumlaumu Mungu kwa sababu tatizo ni la kwetu wala si lake. mfano unamkuta mtu analalamika kwenye maombi yake, na ni wazuri sana kwenye kunukuu maandiko utasikia ulisema tutabarikiwa tuingiapo, tutokapo, litabarikiwa kapu langu!!! ungejua unaemlalamikia kwanza hata kukusikia akusikii ungeacha tu.....Kwaiyo ebu tubadikilike sasa tuache maovu na dhambi tunazofanya kwa hakika baraka zitatujilia, maana Mungu si Mwanadamu hata aseme uongo lazima atafanya.

BARIKIWA!!!!!

Saturday, November 28, 2015

SOMO:LAZIMA TUWE NA NENO LA MUNGU ILI TUWEZE KUSHINDA.

        Bwana yesu apewe sifa, Hamjambo na karibuni katika mwendelezo wa masomo yangu.Leo ninalo somo kama linavyosema hapo juu, kwamba ni lazima kuwa na neno la Mungu ili tuweze kushinda.
        Kwanza kabisa neno ni Mungu mwenyewe, soma Yohana 1:1''Hapo mwanzo kulikuwako neno, naye neno alikuwa Mungu. Kwaiyo, tunadhiirishiwa kwamba neno ni Mungu. kwa mantiki hiyo sasa tunaona kuwa kumbe kuwa na neno ni kuwa na mungu mwenyewe.
        Wengi hatujajua kuwa neno ni mungu na kama tunajua sidhani kama wakristo wa sasa tusingependa kusoma neno. Mimi nashangaa sana, yaani sijui mkristo anaishije eti siku inapita hajasoma neno, kwa upande wangu hua najisikia vibaya sanaaaa. Sikatai zipo sababu zinakubana inapita siku hujasoma neno....sawa! ila hakikisha hiyo sababu kweli inakubalika na Mungu na kwa mkristo aliyesimama kweli kweli  lazima aumie ndani au aone utofauti. kama wewe unaona kawaida basi tambua iko shida ndani yako.
       Tuanze kwa kusoma Mathayo 22:29 inasema''Yesu akajibu akawaambia, mwapotea kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa mungu''. Kwaiyo kumbe hawa masadukayo walikua wanapote akwa sababu yakutokujua maandiko. vipi wewe na mimi ambao leo imekua shida kusoma neno la Mungu, alafu bado unataka eti Mungu akuokoe na majaribu yanayokusonga? sikia Yesu alipokuwa akijaribiwa na ibilisi nyikani, alimshinda kwa neno tu...soma Mathayo 4 kuanzia mstari wa kwanza, utaona kila alipokua anajibu alikua ana refer kwenye maandiko. Sasa unaweza ukaona kumbe hata Yesu ambae angeweza na alikua na uwezo wa kumkemea tu shetani na aondoke ila bado nayeye alihitaji neno ili aweze kushinda sembuse mimi na wewe??????
       Ukisoma tena Zaburi 119:11 inasema''moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije nkakutenda dhambi'' Daudi alijua kuwa neno la Mungu likikaa ndani yake si rahisi kwake kuanguka dhambini. ukisona mstari wa 9 inatuambia kuwa ni kwa jinsi gani kijana atasafisha njia yake.......ni kwa kufuata na kutii neno lake. Kwaiyo utalitiije neno la Mungu kama usomi? Kwaiyo bado tunaona umuhimu wa neno yaan Mungu katika maisha ya ushindi.
       Katika waefeso 6:16-17 inasema'' ipokeeni chepeo ya wokovu na upanga ambao ni neno la Mungu''. Sasa unahitaji nini tena maana vita vyetu si juu ya damu na nyama, kwaiyo kumbe kama skari vitani ukiwa na neno your fully equiped yaan kama ni bunduki unayo, magwanda umevaa, begi la kubebea vitu unalo, mabuti unayo, upanga unao n.k...... Ukisoma Joshua 1:8 uataona kwa anasisitiza kuwa na neno na kulitafakari ila nimefurahishwa anaposema '' Ndipo utakapostawi na kufanikisha njia yako.
       Wapendwa wengi wetu hatuna biblia ambayo ndo silaha ya mkristo na bado wengine tunazo biblia lakini ni jumapili kwa jumapili yaani namaanisha unaisoma jumapili kanisani tena ni kufatisha tu yale asemayo Mchungaji ila baada ya pale ni hadi jumapili ijayo aukama kuna ibada siku za katikati. sasa tunategemea vipi kushinda???? sawa maombi ni silaha ila bila neno ni bure ni sawasawa na mtu ana bunduki ila haina risasi alafu yuko mstari wa mbele vitani!!!!! pata picha nini kitatokea.
       Uko mfano wa watu fulani ambao walikua wanafunga ndoa yao. sasa wakati watu wanatoa zawadi, wengine wakatoa gari, friji, dressing table n.k. ila kuna jamaa mmoja yeye aliwazawadia Biblia, tena aliomba kwa mc na akaongea kuwa hana chochote ila kwa kuwatia moyo maharusi wale wakasome( akataja sura na kitabu wakasome). Maharusi walipofika nyumbani wakaiweka Biblia juu ya kabati na kuisahau. siku moja mama alipokua anasafisha kabati akaikuta na kuikung'uta maana ilikua na vumbi mno. alipokua ana kung'uta akakumbuka ile sura aliyowaambia yule jamaa wakaisome, la haula! si akakuta cheque........yule mama alifurai na kurukaruka , akamwita mumewe pia, mumewe alivyokuja walifurai sana.....baada ya furaha kupungua, jamaa si akaisoma vizuri! oooouuuuhh!!! kumbe tarehe ilikua ishapita. cheque ya milioni kumi!  Huo ni mfano tu kwa jinsi gani hawa watu hawakuona umuhimu wa Biblia.


BE BLESSED YOU ALL......( stay inspired)
   
      
         

Friday, November 27, 2015

SOMO: KWANINI VIJANA WANASHINDWA KUISHI MAISHA MATAKATIFU?

Bwana yesu asifiwe wapendwa, natumai hamjambo na mu wazima wa afya.......Dhumuni la somo hili ni kujua ni kwa sababu gani tuna shindwa kuishi maisha matakatifu.
Kwanza kabisa namshukuru mungu kwa kunipa mafunuo juu ya somo hili, kwa sababu imekua kazi kwa sisi vijana kuishi maisha yanayompendeza mungu. sisemi kwamba mimi naishi maisha matakatifu kwa asilimia mia...hapana!!!! wote tunajitaidi katika fuufikia ukamilifu aliousema bwana yesu kuwa na tuwe wakamilifu kama yeye(MUNGU) alivyo mkamilifu math 5:48......ila wapo ambao ni wakristo lakini imekua historia kwa wao kuishi maisha ya utakatifu yaan kwa maana nyingine ni wakristo jina tu.
UTANGULIZI.
Kwanza kama kijana tambua yafuatayo ili uweze kushinda;
1. KIJANA NI MWENYE NGUVU(kimwili na kiroho)
mithali 20:29 '' fhari ya vijana ni nguvu zao''. 1 yoh 1:14b ''nimewaandikia vijana kwa sababu mna nguvu....'' Kwaiyo hapa tunaona dhairi ya kuwa vijana ni wenye nguvu hata biblia imethibitisha hilo...sasa shetani anajua hilo pia kwaiyo hana mda wakuangaika na wababa au wamama wakati vijana ambao ndio taifa la kesho mpo. anajua thamani uliyonayo kwa ajili ya kanisa na taifa lako na ndo maana anakutafuta usiku na mchana.
2. UJANA NDIO MSINGI WA MAISHA(wakati muhimu)
kipindi cha ujana ndio wakati sahihi wa wewe kufanya maamiuzi(future plans) za maisha. muhubiri 12:1'' mkumbuke muumba wako siku za ujana...kabla hazijaja zile mbaya'' maombolezo 3:27'' ni vyema mwanadamu achukue nira wakati wa ujana''. kwaiyo, bado tunaona shetani anatambua hilo pi na ndo maana anataka akuvuruge kipindi hiki ili usiwe na future nzuri. yohana 21:18'' wakati wa ujana ulikua ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako lakini utakapo kua mzee utainyosha mikono yako na mwingine atakufunga na kukupeleka usikotaka''
sasa tuangalie kwanini tunashindwa kuishi maisha matakatifu.....
1. KUISHI KTK MWILI... warumi 8:13-14''mkiishi kwa kuyafuata mambo ya mwili mwataka kufa bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa roho, mtaishi.....wengi tunashinda kwasababu tunaishi mwilini, atuwezi kushinda bila roho mtakatifu kukaa ndani..
1tim 2:22, math 26:41b''roho i radhi ila mwili udhaifu'' kwaiyo roho inawezekana inataka ila mwili wako bado ni kikwazo..kumbuka paulo alisema nilipendalo silifanyi ila nisilolipenda nalifanya. gal 6:8, efe 4:22-24'' inatuambia mvaeni roho mtakatifu......kwaiyo bila shaka tukimvaa roho sidhani kama habari itakua ni ya kushindwa tu....na hili ndo tatizo kuu kishi mwilini.
2. KUJICHANGANYA
1yoh 2:15,17 tatizo lingine la sisi vijana ni kuipenda dunia.....mstari huu unasema'' msiipende dunia na mambo yaliyomo ndani yake'' sasa unatakaje kuishi maisha matakatifu wakati hutaki kuachana na dunia? ukisha okoka umekua adui wa dunia soma 1yoh 3:13'' msistaajabu ulimwengu ukiwachukia''.
3.MARAFIKI/ MAHUSIANO
sababu nyingine ni marafiki tunaochagua. mara nyingi nasema na imeshawai kunitokea, uchaguzi wa marafiki au mahusiano ulio nayo wanachangia sana katika ushawihi. uwezi ukasimama wakati unaambatana na wasio amini. 2wakorinto 6:14'' usifungwe nira pamoja na wasio amini''. mithali 13:20, 1korinto 15:33, 15:11..........
MBARIKIWE WOTE KWA KUSOMA..........surely something will change after reading this......shalom!!!!!
for more information 0715918940

SOMO: UNAITUMIAJE NEEMA ULIONAYO?

Bwana yesu asifiwe friends, ni matumaini yangu mu wazima wa afya. ni siku nyingine tena ambayo bwana ametuwezesha kuiona. napenda kukushirikisha somo jingine ambalo bwana amenipa.
UTANGULIZI:
Kwanza tuanze kwa kuangalia neema ni nini? katika tafsiri ya kamusi ya kisasa inasema, neema ni mafanikio alionayo mtu kutokana na majaliwa ya mwenyezi mungu au juhudi zake, baraka n.k. kwa tafsiri yangu, Neema ni nafasi ya upendeleo au kuchaguliwa bila kustahili.
Wengi tunafikiri kuwa imetoketokea tu tupo hai hadi sasa hivi, si mgonjwa, si kilema, huna matatizo alafu unajisifu ukidhani wewe unafaa sana mbele za Mungu. kama tulivyoona hapo juu, umependelewa au umechaguliwa bila kustahili.
Hivi fikiria kwa mfano leo Mungu akakutokea alafu aseme anataka kukuchukua pumzi yake au la umpe mabilioni ya pesa!!!! nani angeweza?????.....kwaiyo bado ukijaribu kutafakari unaona kwamba umepewa nafasi(CHANCE) bila kustahili.
ukisoma yakobo 4:6 inasema'' mungu huwapinga wajikuzao bali huwapa neema wanyenyekevu.
waefeso 2:8-9, paulo anasema''kwa maana nimeokolewa kwa neema kwa njia ya imani ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa cha Mungu wala si kwa matendo mtu yeyote asije akajisifu.....heri yake paulo alijua kwamba kuishi kwetu ni neema yake mungu...Wapo watu wanaojisifu. jamani tambueni kuwa umepewa neema na Mungu wala si kwa mapenzi yako ila ni kwa makusudi yake...Nimetoa mfano hapo juu, kwamba kama Mungu angesema tumlipe kwa pumzi yuliyonayo, basi dunia ingekua haina mtu.2wakorinto 1:12, 6:1''Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure....
SASA UNAITUMIAJE NEEMA ULIYONAYO?
tuangalie tena 1Wakorinto 15:10''Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyokuwa kwangu si bure bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote wala si mimi bali ni neema ya Mungu pamoja nami.... Hapa tunaona paulo anasema kwa sababu hivo alivyo ni kwa neema ya mungu basi alizidi sana kufanya kazi kupita wote. Kwaiyo baada ya kutambua kuwa umepewa neema, ni vyema sasa ukaishi katika mapenzi yake kwelikweli maana mda wowote atataka umrudishie pumzi yake.
2Timotheo 2:1''Basi wewe mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu...Anaposema tuwe hodari maana yake ni tufanye kazi ya mungu kwelikweli hali tukijua kuwa neema tuliyonayo hatukustahili. Pia kuitumia vizuri neema yetu ni kuzidi kutenda mema na kuwa watakatifu maishani mwetu.(SISI NI WASAFIRI DUNIANI)
somo hili mungu alinipa kwa makusudi yake na ni naamini kuwa wakristo tuliowengi bado hatujajua kuwa tunaishi kwa neema na neema hiyo tumepewa kwa kusudi lake....Kuna wengine tunaishi maisha ya uvugu uvugu, hatutaki kuwa committed na kazi ya Bwana. Endelea tu kufanya dhambi, maana hata biblia inasema mwenye dhambi na azidi kufanya dhambi na mtakatifu na azidi kujitakasa...sasa wewe utajua ufanyeje maana mtu mzima alazimishwi ila anachuja kabla ajafanja.ni ombi langu kuwa kuanzia leo, ebu tuanze kuitumia neema hii ipasavyo, Mungu anatuangalia tu na kutupima,kuna siku atachukua neema yake na ndipo utajuta kuwa kwa nini uliichezea...soma zaburi103:8-9 anasema''bwana amejaa huruma na neema, haoni huruma upesi, ni mwingi wa fadhili. Kwaiyo Mungu anatuvumilia tu ila ataposema sasa yatosha, Ndugu hakika utajuta.pia ukisoma warumi 2:4-5 inasema'' au waudharau wingi wa wema wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta uapate kutubu... mstari wa tano unasema kwa ugumu wa moyo wako wajiwekea hakiba ya hasira ya mungu katika siku ile ya hukumu.
kwaiyo Ndugu zangu tutumie hii neema vizuri ingali tuliwa hai....
MUNGU AWABARIKI SANAAA!!!!!!
unaweza kunipata pia katika facebook kwa mafundisho zaidi.
shalom!!!!!!!!