Bwana Yesu apewe sifa wandugu..........!
Leo ntaenda kuongelea nguvu za Mungu katika maisha yako.
kama kichwa kinavyosema, inawezekana nguvu za Mungu katika maisha yako hakuna au zimepungua.
Tuanze kwa kusoma Mdo 1:8 inasema " lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajillia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashaidi wangu katika yerusalemu na katika uyahudi wote na samaria na hata mwisho wa dunia" hapo juu nimesema inawezekana huna kabisa nguvu za Mungu au umepungukiwa na hizo nguvu. zipo sababu;
1 HUJAZAZWA ROHO MTAKATIFU
2 ROHO HAYUMO TENA NDANI YAKO
inawezekana umeokoka lakini bado hujajazwa Roho Mtakatifu kwaiyo ni ngumu kuwa na nguvu maana tumesoma pale kwamba mtapokea nguvu akiisha kuja kwenu. pia inawezekana huyu Roho Mtakatifu hayumo tena kwa maana ya kwamba labda ulijichafua kipindi fulani katika maiha yako, ulirudi nyuma naye akakuacha maana wewe ni hekalu lake. na ndio maana tunashauriwa kujazwa maana ziko faida nyingi za kuwa na Roho Mtakatifu.
Sasa tuangalie tena Waefeso 3:20 inasema" basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. kwaiyo kumbe Mungu anafanya kazi kwa kadri ya ngu zilizopo dani yetu!!!! ndio maana yake, sasa jiulize kama wewe huna hizo nguvu za Mungu ndani yako inakuwaje?? kuna umuhimu tena mkubwa sana ya kuwa na nguvu za Mungu ndani yetu. kwaiyo hapa inategemea sasa,
Wafilipi 4:13 inasema" nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu" tunaona tena kumbe tunayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu yaani Roho Mtakatifu. ndio maana nikasema hapo juu iko shida kama huna Roho Mtakatifu na hii imekuwa sababu ya watu wengi kushindwa kiroho yaani kuanguka au kurudi nyuma! andiko linasema tunayaweza mambo yote katika yye atutiaye nguvu, sasa kama huna huyu Roho inakuwaje hapo?
2Tim 4:17 inasema" lakini Bwana alisimama akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu hata wasikie mataifa yote nami nikaokolewa katika kinywa cha simba" paulo anazidi kutuonesha faida za kuwa na nguvu za Mungu ndani yetu.
Nguvu za Mungu ni muhimu sana katika maisha yako mpendwa, kama nilivyosema hapo awali inawezekana hujawahi kujazwa kabisa au Roho Mtakatifu hayumo tena ndani yako. kumbuka Mdo 1:8 kwamba mtapokea nguvu akiisha kuja Roho Mtakatifu katika Maisha yenu. ni ngumu sana kuweza bila kuwa na nguvu za Mungu, wengi wamerudi nyuma, wameanguka maana nguvu za Munngu zenyekuwawezesha hazimo ndani yao kama Wafilipi 4:13.
STAY INSPIRED!!!!!!!!!
Ahsante kwa kunifunza kitu ambacho sikuwa nacho.ubarikiwe sana
ReplyDeleteAMEN BARIKIWA SANA
ReplyDeleteAMEN MTUMISHI
ReplyDeleteTwashukuru
ReplyDeleteBarikiwa sana Mtumishi wa MUNGU kwa neno zuri la kutukumbusha kuhusu Nguvu za MUNGU.
ReplyDeleteBarikiwa sana
ReplyDelete