Tuesday, February 23, 2016

SOMO: NJIA TANO ZA KUMJUA MUNGU VIZURI.


BWANA Yesu apewe sifa wandugu............
Inawezekana umeokoka na Yesu anaishi ndani...ila inawezekana pia haujamjua huyu Yesu vizuri........ kudhibitisha haya soma Marko 4:35-41, utaelewa. ukisoma mstari wa 41 unasema" wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, ni nani huyu hata upepo na bahari humtii?
Hapo tunaona kwamba wanafunzi wa yesu walikua nae siku zote, waliona miujiza yake, ishara na maajabu lakini siku ya dhoruba walishangaa kuona upepo na bahari vikimtii.......!!!! kwaiyo hawakumjua Yesu vizur. nimepata mafunuo katika njia za kumjua Mungu vizur.......fuatilia!
1 KUMTAFUTA KWA BIDII
Mithali 8:17 inasema" nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. hapa anasema kuwa anatupenda...inawezekana unampenda Mungu na kwanza sidhani kama kuna mtu ukimuuliza kama anampenda Mungu atakujibu kuwa Hampendi, wote watasema wanampenda ila ukiendelea anasema wanaomtafuta kwa bidii ndio watakao muona. nikagundua kuwa kuna tofauti ya KUMPENDA, KUMTAFUTA na KUMTAFUTA KWA BIDII. inawezekana unampenda na unamtafuta, sasa nataka uweke bidii ili uweze kumwona. Zaburi 105:4 inasema "mtakeni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake sikuzote......sasa hapa bidii iko wapi? ni pale alipomalizia kwa kusema SIKUZOTE! Mithali 13:4 inasema "nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.
2 KUMTAFUTA KWA MOYO WAKO WOTE
Kuna nyimbo tulikua tunaimba inasema" jesus is number one, is everything to me! sijui kama huwa unamaanisha ukiimba hii nyimbo? Yeremia 29:13 inasema" nanyi mtanitafuta na kuniona, mkinitafuta kwa moyo wenu wote" hapa anamaanisha kuwa u give up everything just to have him. kumbuka Mathayo 6:33, sasa watu wanaigeuza hiyo na kuweka mambo yao mengine mbele.
Kumb 4:29 inasema"lakini huko, kama mkimtafuta BWANA Mungu wako utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote. Mathayo 22:37-38 inasema" akawaambia mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili yako yote. ni ngumu wapendwa kumjua Mungu ipasavyo kama bado hatufanyi kama maandiko yasemavyo....Bwana atusaidie!!!!
3 KULIJUA NENO LAKE
mwalimu anapofundisha wanafunzi darasani huwa anawaachia notes wakasome...unajua kwanini? ili walijue lile somo vizuri kama isingekua ivyo basi ingeishia darasani tu na mtiani unakuja. sasa hivyo hivyo, mafundisho kanisani hayatoshi lazima tuwe na muda wa kumtafuta Mungu kupitia maandiko yaani NENO LAKE! Mathayo 22:29 inasema" Yesu akajibu akawaambia, mwapotea kwa kuwa hamjui maandiko wala uweza wa Mungu. inamaana kupotea kwetu inasababishwa na kutokujua neno la Mungu na kwa kulijua neno la Mungu inatusaidia kumjua zaidi na zaidi. Soma Mithali 2:1-5...mstari wa 5 unasema" ndipo utakapo fahamu kumcha Bwana na kupata kumjua Mungu.
4 KUISHI MAISHA MATAKATIFU
Mungu anaheshimu sana watakatifu...sijui kama unajua hilo! soma Zaburi 25:14 inasema" siri ya Bwana iko kwa wale wamchao, na yeye atawajulisha agano lake" sasa unataka nini tena? neno li wazi Mungu ukiwa karibu na Mungu kwa maana ya utakatifu, utamjua Mungu vizuri. ipo mifano ya kina henoko, eliya n.k.
5 KUWA NA ROHO MTAKATIFU
inawezekana ukawa unaishi kumbe roho alishaondokaga zamani, pengine ulijichafua akakuacha maana we ni hekalu lake! Wakorintho 2:10-11 inasema" lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho, maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu. maana ni nani katika binadamu ajuaye mambo ya binadamu ila roho iliyo ndani yake? vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna afahamuye ila Roho wa Mungu.
Wapenzi Mungu awabariki sana kwa kusoma. usidhani utapoteza mda kwa kusoma, na kwa yeyote atakayesoma somo hili nakuombea sasa;
Mungu anaenda kubadilisha maisha yako na hautakuwa kama ulivyokuwa hapo awali........mwenye matatizo yanaondoka katiika jina la Yesu Kristo, mgonjwa unapokea uponyaji wako sasa, umekosa amani Mungu anakupa amani sasa na hakika utaenda kuuona ukuu wa Mungu katika maisha yako...AMEN
STAY INSPIRED!!!

87 comments:

  1. Replies
    1. amen amen asante kwa neno zuri mtumishi

      Delete
    2. Mungu akubariki mnoo mnoo kwakweli nimefuraiya somo mnooo🤝

      Delete
    3. Amen Amen ubarikiwe sana Mungu akuzidishie

      Delete
  2. Mungu akubariki sana mtumishi nimeipenda hiyo mungu aendelee kukupatia ufunuo tubarikiwe

    ReplyDelete
  3. Amina wapenz wangu Mungu awabariki Sana Sana....kwa kunitia Moyo!!!!

    ReplyDelete
  4. NIMEPATA KITU CHAKUNISAIDIA. MUNGU AKUPE MASOMO MENGINE ZAIDI ILI KULIIMARISHA KANISA. AMEN

    ReplyDelete
  5. Ubarikiwe sana mtumishi kwa somo nzuri

    ReplyDelete
  6. Mungu akubariki Mtumishi pamoja na Kristo hakika nimepokea Mabadiliko ktk maisha yangu

    ReplyDelete
  7. Amina sana nimepata ujumbe mzuri umenibariki Mungu akuinue zaidi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mungu akubariki sana mtu wa imani kwa somo n

      zuri

      Delete
  8. Asante sana Mungu akubariki kwa somo zuri

    ReplyDelete
  9. Amen ...
    Neno la Mungu linaishi...

    ReplyDelete
  10. Amen tubarikiwe San Mtumishi wa MUNGU

    ReplyDelete
  11. Amina mtumishi wa Mungu

    ReplyDelete
  12. Mungu akuinue tena barikiwa

    ReplyDelete
  13. Amee ubarikiwe mtumishi wa MUNGU

    ReplyDelete
  14. Amina,barikiwa sana

    ReplyDelete
  15. Asante kwa neno barikiwa

    ReplyDelete
  16. ubarikiwe, umenifanya nichukue notes kabisa ili nipate kujisomea mara kwa mara

    ReplyDelete
  17. Mungu akubariki sana brother

    ReplyDelete
  18. Amen mungu akubariki ndugu

    ReplyDelete
  19. Mungu akubaliki sana

    ReplyDelete
  20. AMEN.... BLESSED ALOTS 🙌

    ReplyDelete
  21. Amen, barikiwa sana mtumishi wa Mungu

    ReplyDelete
  22. Barikiwa sana Mtumishi wa Bwana Yesu Kristo
    KUMJUA MUNGU NI ZAIDI YA KUWA NA MAARIFA YA DUNIA HII

    ReplyDelete
  23. Mungu akubariki, ahsante kwa huduma

    ReplyDelete
  24. amina ubarikiwe na Bwana kwa fundisho la baraka

    ReplyDelete
  25. Asante sana mungu akulide umenielinisha sana heko sasa nimepata ujuzi

    ReplyDelete
  26. Mtumishi umeandika kweli ya kumjua mungu , mungu amekuinua na azidi kukushushia mungu roho mtakatifu🙏

    ReplyDelete
  27. MTUMISHI WA MUNGU, NIMEBARIKIWA SANA NA HIZI FAIDA AU NJIA ZA KUMJUA MUNGU ZAIDI.
    Mungu akuinue zaidi Mteule wa Yesu.

    ReplyDelete
  28. Kutembe katika njia za mungu so powerful indeed

    ReplyDelete
  29. Abarikiwe Sana nimefunguliwa kupitia Neno hili!!

    ReplyDelete
  30. Ubarikiwe sana mtumishi was mungu aliyehai, nimejengeka

    ReplyDelete
  31. Barikiwa sana mtumishi,Limekuwa ni neno la wakati kweli

    ReplyDelete
  32. Napokea katika jina ya yesu

    ReplyDelete
  33. Thanks God bless you

    ReplyDelete
  34. Mungu akubariki sana kwa ujumbe wako mzr toka kwa mungu

    ReplyDelete
  35. Mungu akubarik mtumishi nimealikiwa sana sana

    ReplyDelete
  36. Cool and that i have a neat provide: How Much Home Renovation Cost house renovation companies near me

    ReplyDelete
  37. Binafsi nimepata uelewa Mkubwa sana Kwenye namna ya mjua Mungu Asante sana.

    ReplyDelete
  38. Ubalikiwe sana Kwa SoMo zuli nimebalikiwa sana

    ReplyDelete
  39. Amen balikiwa mtumishi wa mungu

    ReplyDelete
  40. Ameen ubarikiwe pia

    ReplyDelete
  41. Mungu akukumbuke kwa Chakula kizuri usitawi na kufanikiwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Be blessed man of MOST HIGH GOD

      Delete
  42. Ameeeen Ameeeen
    Mungu akubariki sana

    ReplyDelete
  43. UbalikUba na mungu

    ReplyDelete